Saturday, February 2, 2013

TAMKO LA SHURA YA MAIMAMU MTWARA KUHUSIANA NA ZIARA YA WAZIRI MKUUNdugu wanananchi,waislam na wasio waisalm,amani ya mwenyezi mungu iwe juu yenu..


Kama mlivyo tutuma kwenda kuwawakilisha kuongea na mh. waziri mkuu leo tumekuja kwenu kuleta mrejesho mfupi wa yale tuliyozungumza na mh Wazir mkuu,,

Kwanza kabisa,msimamo wetu upo vile vile kama awali,suala la gesi liangaliwe kwa umakini wa hali ya juu na utekelezaji wake sharti uzingatie malalamiko ya wananchi,tamko letu sisi liko vile vile.

Kwa kuwa katika vile vipengele vyote tulivyoongea na mh. waziri mkuu ni kipengele kimoja tuu katika yale madai yetu kilichofanyiwa kazi,nacho ni kile cha mkuu wa mkoa kuomba radhi kwa wananchi,kwani mkuu wa mkoa kafanya hivyo.

Lakini katika vipengele vyote vilivyobakia serikali haijafanya chochote cha kuturidhisha,kwa hiyo sasa,tunatamka rasmi hatukufikia mwafaka na wazir mkuu..

Kwa mantiki hiyo sasa shura ya maimam inatoa angalizo kwenu wananchi waislam na wasio kua waislam kwa wakati huu tuwe watulivu,tusifanye fujo wakati shura ya maimam inaendelea na vikao na kutoa utaratibu wa kipi kitachofuata,vikao vinaendelea,,juma pili pia kutakuwa na kikao cha mwisho,na kikao cha juma pili kitatoa tamko la jumla ya nini kifanyike na kuangalia mwelekeko upi tuufate.

Tunawaomba sana wananchi tuwe watulivu,tusifanye fuzo za aina yoyote kwa mtu yeyote,tusiharibu mali ya mtu yeyote,tusiharibu mali za serikali na mtu yeyote,tuwe watulivu na tunawaomba tusirudi kule kwenye matukio ya wiki zile zilizopita.

Tungependa kupinga suala hili la gesi bila kufanya fujo na vurugu,,

"To protest without violence",,wasije wakapata sababu ya kusema ya kwamba tunachochea machafuko na uvunjifu wa amani,,

No comments: