Saturday, February 2, 2013

SALAAM KWA DR. W .P. SLAANa The Big Show,


Salaam nyingi sana Dr Slaa,,,


Awali ya yote ni matumaini yetu ya kwamba umzima wa afya na unaendelea vyema na shughuli za kila siku za kujenga chama kwa maslahi ya ukombozi wa taifa hili.

Bila kukuchosha,naomba nichukue fursa hii kuongea nawewe japo kwa uchache kukujuza mambo jins yalivyo na uhalisia ambao ndugu mizengo pinda na rais jakaya mrisho kikwete wanausimamia katika kupotosha taifa hili,tena TUKUAMBIE wazi wazi kwa maslahi ya taifa letu,

Dr slaa,sisi kusini hatuna wa kumlaum zaid ya kujilaum nafsi zetu,tunasema hivi Dr Slaa kwa kuwa ni sisi wenyewe kwa upumbavu wetu tumeiweka madarakan CCM miaka nenda miaka rudi,

Ni sisi wenyewe wana kusini na ulimbukeni wetu tumekua tunaicheza ngoma ya mafisadi kwa kukubali kupewa kanga,vilemba na ubwabwa pasi na kuhoji future ya maisha yetu na vizaz vyetu,,

Ni sisi wenyewe wana kusini kwa ulofa wetu tumekuwa tunakubali propaganda za kishenz za mafisadi ya kwamba CHADEMA ni chama cha kikanda, CHADEMA ni chama cha kikabila,chadema ni chama cha kidini,,

Ni sisi wenyewe wana kusini tumekuwa wapuuzi na kukubali unafiki wa ccm ya kwamba CHADEMA kinataka kuigawa nchi hii eti tuh kwa kuingalia ile sera ya majimbo,haya na mengine mengi dr slaa ni sisi wenyewe tumejitakia,,

Leo hii Jakaya Kikwete amekuwa ni mtu asie sikia na kusahau moja kwa moja ahadi zake alizokazitoa yeye mwenyewe pindi alipokuja kuomba kura huku na sisi tukampa kwa kishindo,,

Leo hii Jakaya Kikwete amekuwa ni mtu wa kuja kudeploy jeshi letu la wananchi lije lipigane na sisi wananchi eti kisa tunaandamana kwa amani na kudai kujua hatma ya maisha yetu,,

Leo hii Jakaya Kikwete na serikali yake imethubutu kutuita sisi ni wanafiki na wahaini eti kisa tunahoji future ya nchi yetu na kizazi chetu,,

Inasikitisha sana Dr Slaa,na inahuzinisha nchi hii kuendeshwa kiholela na kishkaji pasi na kuangalia mipango ya baadae ya maendeleo ya nchi hii,,

Ccm na mafisadi wamekua sio sikivu,wameweka pamba maskion,hawaambiliki na hawaskiii,hawaoni kabisa huku mtwara ni sehemu ambayo kunakuja kutokea machufuko ya kutisha ndani ya nchi hii.

Lengo letu ni kukufahamisha ya kwamba kauli zilizotolewa na mizengo pinda na jakaya kikwete ya kwamba ya mgogoro huku kusini wameumaliza si za kweli,kama una uwezo fanya ziara uje kusini ujionee mwenyewe uhalisia ulivyo.,

Pinda amempotosha rais,na rais pasi na kufikiri kwa upeo wake kakubali upotofu huo na kumpongeza pinda eti ya kwamba kafanya kazi kubwa,iliyotukuka ya kufanikiwa kuumaliza mpasuko huku kusini hali ya kuwa ni kama amezid kuuchochea zaid..

Shura ya maimam kama wadau ambao walifanikiwa kuonana na kuongea na Mizengo Pinda wametoa msimamo wao ya kwamba hakuna makubaliano yoyote ya maana baina yao na pinda na kwamba mgogoro uko pale pale..

DR SLAA,ikukumbukwe ya kwamba Mizengo pinda alipofanya ziara yake kuja Mtwara alionana na magroup mbali mbali ya wawakilishi wa wananchi,,

1.ALIONANA NA BARAZA LA UWAKILISHI WA WAKRISTO LA KIPENTEKOSTE MTWARA NA KUONGEA NAO,

2.ALIONANA NA SHURA YA MAIMAM MTWARA NA KUONGEA NAO,

3.ALIONANA NA WANAHARAKATI WA ASASI ZA KIRAIA NA KUONGEA NAO.

Hao wote ni wawakilishi wa wananchi katika kufikisha ujumbe kwa serikali hii,na makubaliano yaliyakawepo baina yao na Mizengo pinda ni kwamba Mizengo pinda aliyakubali na kuyachukua maelezo yao na kuahid ya kwamba yeye si mwenye kauli ya mwisho,mwenye kauli ya mwisho ni Rais jakaya kikwete na atamshauri kisha atatoa mrejesho,na kwa maana hiyo Pinda akawaomba wawakilishi hao kuongea na wananchi na kuwaasa watulie,wasifanye vurugu malalamiko yao yanashugjhulikiwa..

Cha kushangaza baada ya hapo,Pinda aliporudi Dsm kakimbilia kwenye vyombo vya habari na kusema ya kwamba mgogoro kaumaliza,kakimbilia bungeni na kuongopa ya kwamba mgogooro kaumaliza hadi kafikia hatua ya kutoa ushawishi wa kutoundwa kwa KAMATI TEULE YA BUNGE KUJA MTWARA KUTUSIKILIZA NA KWENDA KUYAZUNGUMZA HAYO BUNGENI..

HUO NI UPOTOFU WA HALI YA JUU SANA ALIOUFANYA MIZENGO PINDA NA DHARAU YA HALI YA JUU SANA KWETU,NA KWA WAWAKILISHI WETU WOTE HAO AMBAO WALIAMUA KUCHUKUA MUDA WAO NA KUKAA CHINI KUMSIKILIZA..

TUNAKUOMBA DR SLAA KAMA KIONGOZI WETU WA JUU WA CHAMA,LICHUKUE HILI KATIKA PICHA YENYE UHALISIA,USIPOTOSHWE NA MAFISADI NA KUFIKIRI YA KWAMBA HUKU MGOGORO UMEKWISHA,NI UONGO WA HALI YA JUU,HUKU HALI BADO NI TETE,NA PINDA KAZIDISHA ZAID HALI HII KUWA TETE PAMOJA NA TAMKO LA HOTUBA YA RAIS IMEZID KUHARIBU MOOD ZA WATU WA HUKU KWA UJUMLA,,

KUBWA TUNALOKUOMBA DR SLAA NA VIONGOZI WOTE WENYE UCHUNGU NA NCHI HII NA RASILIMALI ZETU NI KWAMBA TUNAITAKA KAMATI TEULE YA BUNGE IJE MTWARA,KWA NGUVU ZENU NA USHAWISHI KAMATI HIYO IUNDWE NA IJE MTWARA KUWASIKILIZA WANANCHI IKIWEZEKANA KWA KUPITIA WAWAKILISHI WETU WALE WALE ILI TAIFA LIONE NI JINSI GANI PINDA ALIVYOIPOTOSHA HOJA HII,,

PIA TUNAKOMBA DR SLAA UFANYE ZIARA YA KUJA MTWARA NA KUSINI KWA UJUMLA KUJA KUZUNGUMZA NA WANANCHI WAKO NA WAPIGA KURA WAKO WA 2015 AMBAO KWA NAMNA YOYOTE HAWANA TENA SABABU YA KUENDELEA KUIPA NAFASI CCM NA MAFISADI KWA DHULMA NA UFISADI MKUBWA WANAOENDELEA KUUFANYA KATIKA TAIFA HILI,,

DR SLAA,KWA UFUPI CCM NA MAFISADI WANAUNG'ANG'ANIA MRADI HUO KWA KUWA WASHACHUKUA CHAO NA KUWEKA USWISS NA SASA WANATAFUTA NJIA NZURI YA KUZID KULA RASILIMALI ZETU ILI WAKISTAAFU WAISH KAMA PEPONI WAO NA VIZAZI VYAO NA KUIACHA NCHI HII KWENYE DIMBWI LA UMASKINI..

TUNAKUTAKIA KILA LA HERI DR SLAA KATIKA KUJENGA CHAMA CHETU,NA KATIKA HARAKATI ZA KUHAMASISHA UKOMBOZI WA TAIFA LETU..

KUSINI TUMEJIFUNZA SASA KUTOKANA NA MAKOSA YETU,MSITUCHEKE,MSITUDHARAU,SI SI WOTE NI WA MOJA,

SISI SOTE NI TAIFA MOJA,INAPOBID KUUNGANA BASI TUUNGANE ILI KULIJENGA TAIFA LETU..

TUNAMALIZA KWA KUSEMA YA KWAMBA MGOGORO NDIO KWANZA UNAANZA NA HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE.

IN CHADEMA WE TRUST...!!JAMII FORUMS

No comments: