Tuesday, January 8, 2013

VIONGOZI WA MUUNGANO WA VYAMA VYA SIASA VINAVYORATIBU ZOEZI LA KUHAMASISHA WANANCHI KUHUSU GESI WAKAMATWA NA POLISI

Viongozi wa Muungano wa vyama vya Siasa vilivyokuwa vikiratibu zoezi la kusimamia mjadala wa gesi kutoka ama kubakia Mtwara wamekamatwa na Polisi. Viongozi wa vyama hivyo walikuwa wakiihamasisha jamii juu ya umuhimu wa rasilimali hiyo kwa manufaa ya wananchi wote waishio maeneo ya Mtwara na Lindi. Haijajulikana wamekamatwa kwa kosa lipi ila kwa ubashiri tu yawezekana muungano huo umekuwa tishio na mwiba mkali kwa serikali hasa kufuatia suala hili la maandamano ya kupinga gesi isitolewe Mtwara. Viongozi hao ni wenyeviti na makatibu wa vyama vote vya siasa mkoani Mtwara.Taarifa itatolewa rasmi baadae.

UPDATE

Viongozi hao waliitwa na kuhojiwa na Polisi kisha wakaruhusiwa

No comments: