Monday, January 28, 2013

UPDATE: ZIARA YA WAZIRI MKUU MTWARA

Update:
Majumuisho ya ziara ya Waziri Mkuu yatatolewa tarehe 29/01/2013 siku ya jumanne saa nne asubuhi. Mwakyembe, Magufuli, Kigoda na mawaziri wengine wanne kuwasili kuja kujibu hoja za wananchi.

Waziri Mkuu alikuwa akutane na Waandishi leo saa tisa alasiri. Kutokana na kikao kirefu cha madiwani wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Mtwara vijijini pamoja na kikao cha wafanyabiashara, majumuisho ya ziara ya Mtwara atayatolea ufafanuzi kesho. Kwa sasa anakula chakula na kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mtwara kitafuatia. Kutokana na kuwepo kwa makundi katika Kamati ya siasa ya CCM mkoa, wabashiri wengi wanasema kikao hicho kitakuwa na mvutano mkali.

Dondoo Muhimu
  • Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa bomba la gesi lisiende Dar

  • Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka Waziri Mkuu aondoke naye

  • Wajumbe (Madiwani )kumpinga kwa kauli moja  Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa kutumia mamlaka  kutoa kauli za uongo kuhusu Mtwara vijijini kuunga mkono suala la gesi iende Dar madiwani waMtwara vijijiniwamesemahawakushirikishwa.

  • Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani na Mkuu wa Wilaya
  • Waziri Mkuu kutumia mbinu ya kisiasa kuwashawishi bomba liende Dar
  • Wajumbe wameondoka kwa shingo upande kwa kukubali kutokubaliana na Waziri Mkuu.
  • Kikao kinafanyika chini ya ulinzi Mkali wa FFU, JWTZ na Usalama wa Taifa.
  • Hawa Ghasia arudishwa uwanja wa Ndege JKNIA asije Mtwara kwani anaweza kuchafua hali ya hewa.

  • Polisi wanadai Meya anataka kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana na kauli yake ya kusema wao ndio chanzo cha vurugu.

No comments: