Monday, January 28, 2013

PINDA ,MWEMA,NCHIMBI WAWASILI MTWARA


Update:
Pinda kukutana na waandishi wa habari mtwara leo saa tisa alasiri kutoa majumuisho ya ziara yake.
Viunga vyote vya masasi vimejaa askari polisi, FFU na mbaya zaidi  ni kuona askari wa jeshi la wananchi wa Tanzania wakiwa wamevaa sare wakiranda mitaani na ktk njia za kuingilia na kutokea mji wa masasi.


Pinda na ujumbe wake akiwamo CDF wa JWTZ wapo Masasi kutathmini athari za machafuko toka asubuhi leo hii.
Waziri Mkuu amewasili jana akiwa na ujumbe mzito wa viongozi waandamizi wakiwamo waziri wa ulinzi na IGP. Lengo likiwa ni kutafuta suluhu. Mkutano ulifanyika VETA chini ya ulinzi wa askari wa JWTZ. Jibu alilolipata ni kwamba GESI HAITOKI MTWARA.


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya siasa  na viongozi wa Asasi mbalimbali   kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara Januari 27, 2013


No comments: