Monday, January 28, 2013

NUKUU YA MWANAJIOLOJIA KUHUSU GESI

Ajira sio kitu muhimu hata kidogo, wanamtwara watafaidi sana kupata umeme wa uhakika na wa bei nafuu utakaokuwa kivutio kwa uwekezaji Mtwara. Pia gridi mpya ikijengwa kusafirisha umeme kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, mikoa ya Mtwara na Lindi itakuwa imeunganishwa na gridi ya taifa na hivyo kuwa na mifumo ya umeme yenye uhakika zaidi na hivyo kuboresha kasi ya uwekezaji.


Gharama ya kusafirisha umeme ni karibu mara mbili ya gharama ya kusafirisha gesi lakini cha muhimu hapa ni jumla ya faida zote zitakozopatikana kwa kipindi chote cha uhai wa mradi ambazo ni kubwa sana iwapo umeme utazalishwa Mtwara na kusafirishwa kwa gridi hadi Dar es Salaam ukilinganisha na jumla ya faida zitakazopatikana kutokana na gesi kusafirishwa kwa uzalishaji umeme Dar. Wataalamu wetu wanatakiwa kutoa ushauri fasaha kwa viongozi wetu wa kisiasa vinginevyo itakuwa aibu. Hata ambaye hakwenda shule kabisa anaelewa chaguo ni lile linalotupatia faida kubwa zaidi na sio gharama ndogo zaidi kwa kipindi chote cha uhai wa mradi.


-DR. ANTIPAS MASSAWE

No comments: