Tuesday, January 29, 2013

MAJUMUISHO YA YA ZIARA YA DHARURA YA WAZIRI MKUU MTWARADONDOO MUHIMU KATIKA MAJUMUISHO
  • Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Simbakalia kawaomba radhi wananchi wa Mtwara.
  • Waziri Nchimbi kutumia lugha kibabe na vitisho dhidi ya raia pamoja na taarifa isiyokuwa na tathmini halisi na yenye uwiano pale alipotolea mfano askari aliyevamiwa dukani/baa yake na kuibiwa pesa kiasi cha sh. 1,895,oo/= na Kupoteza mali ya sh 200,000,00/= (milioni mia mbili) na kusababisha watu wagune.
  • Kawambwa kawahimiza wazazi kuwaruhusu watoto kwenda shule kupata elimu sanjari na chuo cha VETA kutoa masomo ya mitaala ya gesi sanjari na uchomeleaji baharini.
  • Tibaijuka amezungumzia kuhusu upanuzi wa mji wa Mtwara na kuleata kauli mbiu ya "Amani na maendeleo" kutoka kwao Kagera.
  • Mwakyembe amezungumzia  upanuzi wa bandari kavu na ujenzi wa reli Mtwara, Liganga, Mchuchuma hadi  Mbamba bay na kuahidi kuja Mtwara kila baada ya miezi 3 na kujadili na kutathmini changamoto.
  • Waziri Mkuu ametoa udhuru wa waziri wa ujenzi Dr Magufuli ambaye alitakiwa kuwepo lakini hataweza kuhudhuria.
  • Bi Mapunjo kaahidi mipango mikubwa ya ujenzi wa viwanda mkoani Mtwara.
  • Mbilinyi kaainisha idadi ya makampuni yaliyoonyesha nia ya kuja kuwekeza Mtwara (Sina hakika sana kama ni Mtwara).
  • Waziri Mkuu katoa majumuisho ya ziara yake ambayo hayana tofauti na haya yaliyojadiliwa.
  • Kwa ufupi ni sarakasi, sanaa, ngonjera, kwaya na maigizo hakuna jipya.Habari ya video itakujia baada ya kuhaririwa.

No comments: