Thursday, January 10, 2013

KUMBU KUMBU YA REGIA MTEMA

Siku ya Jumatatu; tarehe 14 January 2013 ni siku ambayo Regia Mtema Foundation imeitenga maalumu kwa ajili ya kumbukumbu ya Regia Mtema. Katika siku hii maalumu wote mnakaribishwa Peacock Hotel ambako kutakuwa na maada mbalimbali zitakazowasilishwa na kujadiliwa kama alivyozisimamia Regia. Katika siku hii maalumu wageni na wadau mbalimbali wamethibitisha kushiriki.


Hafla hii maalumu itaanza saa 9.00 Alasiri na kumalizika 2.00 usiku na kisha kufuatiwa na chakula cha usiku. Ratiba kamili itahusisha matukio yafuatayo:


Historia ya Regia itakayowasilishwa na Mh. David Kafulila

Mada juu ya Rushwa itakayowakilishwa na Takukuru

Ulemavu Siyo Kutoweza itakayowasilishwa na Bi Shida Salum - Mwenyekiti CHAWATA

Nafasi ya Kijana katika kuchochea maendeleo na demokrasia - Mh. January Makamba

Majadiliano

Documentary za Regia Mtema

Remarks kutoka kwa Mh. Zitto Kabwe; Mh. John Mnyika na Hussein Bashe na Mzee Mtema

Chakula cha jioni

NetworkingWasimamizi wa hafla hii watakuwa: Pascal Mayalla na Lara Williams


Thibitisha kuhudhuria kwako kwako kupitia number: 0713 694 820


CC: Pasco; lara 1; Mzee Mwanakijiji - Naomba msambaze mwaliko huu.

Wasalaam

Sanctus Mtsimbe

Mwenyekiti; Regia Mtema Foundation

Sokoine Drive/Pamba Road

Opposite Luther House or Life House/Tancot House;

2nd Floor; Left Wing (3rd Floor including Mezanine)

No comments: