Friday, January 11, 2013

JESHI LA POLISI LAFUNGA MADANGURO YA MWANANYAMALA

Jeshi la polisi mkoa wa Kipolisi Kinondoni jijini Dar es salaam limeyafunga madanguro yaliyopo Mwananyamala na kuwakamata akinadada 35 waliokuwa wakiuza miili yao pamoja na Cesilia Vitalis, mama wa miaka 70 ambaye anadaiwa kuwa ndiye mmiliki wa madanguro hayo.MTAZAMO:
Ashakum si matusi miaka ya 60 na 50 Kisutu ilikuwa inasifika kwa aina hii ya madanguro na wahusika walikuwa wanatoke mkoa maarufu unaozalisha kahawa kanda ya ziwa.

Na utaratibu huu umeendelea isipokuwa miaka ya 80 ulitibuliwa na ugonjwa wa Ukimwi. Hata hivyo mtindo huu bado unaendelea na maeneo yanajulikana. Na mapolisi hutumia kama vichaka vyao vya kupokea rushwa. Maeneo yanayosifika kwa biashara hii ni Tandale, Uwanja wa fisi, Buguruni kwa Mnyamani, Temeke. Pia pombe za gongo na zile za kienyeji pamoja na madawa ya kulevya huambatana navyo. Maeneo yanajulikana lakini yanafumbiwa macho.

Kama Polisi wanataka kufanya "crack down" kulizima hili tatizo waanze na suala la watoto kuzurura, Omba omba, madanguro pamoja na wale wanaojiuza barabarani, wakabaji wa pale Ubungo, Jangwani , Tandale kwa Ali Maua, Tandika n.k Sio kujionyesha kwenye TV na kutaka umaarufu. Kimsingi hivi ni vichaka vyao vya kula rushwa na hii imetokana na "Public outcry" ya wananchi wanaozunguka maeneo hayo kukerwa na vitendo hivyo. Hizi kero ziwe za kitaifa. Kila mtu kuanzia juu mpaka chini afanye kazi kihalali mathalan Ufisadi.No comments: