Wednesday, November 7, 2012

JEURI YOTE HII WAMEIPATA WAPI?
Na Baraka Mfunguo,

Ni wiki kadhaa sasa tumekuwa tukiishuhudia kadhia hii ya wachuuzi wa mafuta inavyoleta athari kubwa ya kiutendaji pamoja na kiuchumi na athari zikionekana waziwazi. Hivi sasa mafuta yamekuwa bidhaa adimu na sio kwamba ni adimu kwamba yamekuwa adimu isipokuwa yameadimishwa na baadhi ya watu kwa maslahi yao na maslahi ya matumbo yao.

Hivi watanzania tumekwisha fikia hatua ya ubinafsi kiasi hiki? Walianza kwa kuchakachua mafuta.... Mpaka magari ya viongozi yakaingia mkumbo. Lakini   inawezekana na serikali  nayo ina udhaifu wake ni kama imefumba kinywa , imefumba mikono na kuziba masikio kana kwamba mambo hayo yanafanyika nchi ya jirani.

Imefikia hatua mpaka watendaji wa serikali ambao wameingia mikatab ya zabuni za kupata mafuta katika makampuni wakilishwa ya wachuuzi hawa kutukanwa matusi. Ndio ... wamefikia hatua ya kuitukana serikali matusi.... JEURI HIYO WAPEIPATA WAPI? (Wewe mmiliki wa CENTRAL BELT PETROL STATION MTWARA unapewa jeuri na nani wewe? ama na Majogo kama wanavyosema mtaani ? Usitutishe, usitubabaishe, hauko peke yako nchi hii wewe ni sawa sawa na punje mbele ya umma  wa watanzania)

Au ina maana kuna baadhi ya watendaji wakubwa serikalini wana mkono wao na ndicho kinachowatia kiburi? Ama ni amani na utulivu wa watanzania ndicho kinachowatia kiburi.. ama ni fedha zao ndizo zinazowatia kiburi...Nadhani kwa sasa imetosha . Serikali inapaswa kuchukua hatua ama iwaachie watanzania waamue kuchukua hatua... Hivi tujiulize haya ndiyo matunda ya soko huria/soko holela ama ni hila za baadhi ya watu? Mamlaka zinazohusika...Wizara ya Nishati na Madini, EWURA, TPDC, TRA wako wapi? Ama na wao wametiwa mifukoni hawana pa kutokea. Kwa nini Watanzania tuteseke namna hii.... ? Tumewakosea nini hawa....

Nadhani dhamira yao kuu ni moja, ni kujinufaisha wao, hakuna mwingine isipokuwa wao tu kwa sababu wao wanajiita wafanyabiashara na kama mfanyabiashara huhitaji kufanya biashara yake kwa faida. Sasa kama hawapati faida mbona bado wanaendelea nayo? Ama ndio "delay tactic" wanayotaka kutuletea? Wanataka kutufanya wajinga kiasi cha kuwaona watanzania wote ni wajinga.. Wanataka kuharibu uchumi wa nchi ,wanataka kuharibu pia njia kuu za uchumi wa nchi, wanataka kufanya hata kile kidogo kilichofanyika kisionekane, wanataka kumwonyesha Rais aliyepo madarakani kwamba yeye hana nguvu isipokuwa wao. Kwani Rais huyu si kiongozi wa Watanzania? Ama na yeye watasema wamemweka mfukoni? Inawezekana wakajipa matarajio hayo lakini si kwa watanzania wenye akili timamu.

Hatua za kuchukua

  • Serikali itaifishe visima vyote vya mafuta pamoja na vile ambavyo vimehodhiwa na baadhi ya watendaji wa serikali baada ya kukiua kiwanda cha TIPER.

  • Taarifa zote za kuingia mafuta ghafi pamoja na manunuzi yake ziwekwe wazi ili watanzania wote wajue. Kama inavyofanyika katika vyombo vya habari vya kimataifa ambapo huweza kueleza na njia hii huweza kuwasaidia wabashiri wakubwa wa uchumi. Sio hilo tu, hata gharama ya viwango vya dhahabu pia viwekwe wazi. Watanzania sio wajinga tena. Wanataka kuvifanya hivi vitu viwe vya siri siri kwa faida yao. Lakini kwa kweli wanatuchezea kwa kiasi kikubwa.

  • Hawa wachuuzi wa mafuta walipo mikoani na kwenye majiji wachukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na kufutiwa leseni zao pamoja na za mabwana zao wanaowatia viburi ambao ni waagizaji wakubwa wa mafuta. Vinginevyo watanzania wachukue hatua.

  • Sheria ya uhujumu uchumi ifufuliwe kama ilikuwa imekufa ama ina mapungufu basi ipitiwe upya. Ili iweze kuwabaini hawa wanaowatia kiburi hawa wachuuzi wa mafuta ni akina nani. Ikiwezekana wapigwe risasi ama wafungwe maisha.

  • Kwa sababu hawa wanafanya matukio haya kwa makusudi, hususan pale serikali inapokuwa inatafuta mbinu thabiti za kuweza kutoa haki sawa kwa wote yaani wasambazaji/wazalishaji "suppliers" na wale walaji/watumiaji "consumers ama Domestic House Holds". Na kupelekea  wao kuyapinga maamuzi hayo kwa sababu zao binafsi. Na kufanya maamuzi ambayo yanataka kuisababishia serikali hasara na maafa. Basi pasina shaka lolote hawa ni WAHAINI. Na sheria ya UHAINI ifuate mkondo wake.

  • Waziri wa Nishati na Madini aingilie kati kuitatua kadhia hii. Tunatambua umahiri wake na weledi wake na inawezekana akakwamishwa na vikwazo fulani fulani, lakini sio watanzania ambao wanajua umahiri wako. Kazi yako ni moja tu ingawa sikufundishi kazi yako. Ni kubaini mianya pamoja na kasoro zote na kuzifutilia mbali kabisa.

  • Mwisho , Mkurugenzi wa TPDC na EWURA wajiuzulu/ wawajibishwe kwa uzembe. Pamoja na kupitia upya sheria zilizounda mashirika haya pamoja na mashirika mengine yaliyopo katika Wizara ya Nishati na Madini. Ili ikiwezekana vyombo hivyo vifutwe na viundwe vingine ambavyo vitaleta ufanisi katika utendaji wa nchi.


MSITUFANYE MABWEGE TUMEWACHOKA NYINYI WACHUUZI/WALANGUZI WA MAFUTA. TOKENI KATIKA NCHI YETU WANYONYAJI/WEZI WAKUBWA NYINYI MSIOKUWA NA UTU WALA UZALENDO KWA NCHI YENU.

No comments: