Thursday, October 25, 2012

WANNE MBARONI DAR KWA MAUAJI YA ALIYEKUWA RPC WA MWANZA
KIKOSI maalumu cha vyombo vya usalama chini ya Jeshi la Polisi, kimewatia mbaroni jijini Dar es Salaam watuhumiwa wanne muhimu wa mauaji ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.Habari za uhakika zimethibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao muhimu ambao wanatarajiwa kuhojiwa na kusafirishwa kwenda Mwanza kushitakiwa.


Barlow enzi za uhai wake

Gari aina ya HILUX (T 777 BFY) linalodaiwa hayati RPC Liberatus Lyimo Barlow wa Mwanza, alikuwa akiendesha siku mauti yake yalipomkuta kwa kuuawa papo hapo kwa kupigwa risasi na watu wanaosadikiwa kuwa ni MAJAMBAZI Kitangiri Jijini Mwanza Tar 13/Oktoba/2012.

Gari hilo linalodaiwa kuwa ni mali ya RPC Barlow likiwa limeegeshwa katika moja ya vituo vya Idara ya USALAMA jijini Mwanza!HABARI NA PICHA : FIKRA PEVU

No comments: