Wednesday, October 31, 2012

WANANCHI WANAHAMASISHWA KUCHANGIA DAMU KWA HIARI KUOKOA MAISHA YA WAGONJWA WANAOHITAJI DAMU HOSPITALINI


Mpango wa Taifa wa Damu salama Unatoa WITO kwa wananchi kujitokeza kuchangia damu kwa hiari kwenye vituo vya damu salama

Damu ni Uhai na inahitajika, mahitaji ya damu nchini ni wastani wa chupa 400,000 kwa kipindi cha oktoba 2011- Septemba 2012 mpango umekusanya chupa 110,000.

Upungufu wa damu katika vituo vya damu salama husababisha wagonjwa kupoteza maisha kwa kukosa damu au kutopata damu kwa wakati, vifo ambavyo vinaweza zuilika kama watanzania watajenga utamaduni wa kuchangia damu mara kwa mara

Upungufu wa damu unatokana na sababu zifuatazo;

• Uelewa mdogo wa wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia damu kwa hiari

• Kuenea kwa maambukizi ya ukimwi, hivyo kusababisha watu kuwa waoga kuchangia damu

• Uuzwaji wa chupa za damu mahospitalini kunakofanywa na watumishi wasio waaminifu hivyo kukatisha watu tama

• Imani potofu katika jamii kuhusu uchangiaji damu Mfano uchangiaji damu unaweza kusababisha kupata maambukizi kitu ambacho si kweli

Wananchi wanaombwa kutembelea vituo vifuatavyo kuchangia damu;

Mwanza- karibu na Hospitali ya Bugando

Tabora – karibu na Hospitali ya kitete

Dar-es-salaam- ilala mchikichini, hospitali ya lugalo, kituo kidogo cha mnazi mmoja

Mbeya- karibu na Hospitali ya Meta

Kilimanjaro- Karibu na Hospitali KCMC

Mtwara- karibu na Hospitali ya Ligula

Lindi- kituo kidogo karibu na uwanja wa ilulu

Dodoma – kituo kidogo nje ya Hospitali ya mkoa (Jenero)

Morogoro- Kituo kidogo karibu na Hospitali ya mkoa

Kagera- kituo kidogo

Na Hospitali nyingine yoyote ambayo inatoa huduma ya kuongeza damu

Kwa maelezo zaidi piga simu namba 0222181873 au 0712612000

Kumbuka; Inawezekana damu unayochangia ni kwa ajili yako, familia na jamii

Pichani ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Bwana Leonidas Gama akichangia katika kituo cha damu salama Kilimanjaro siku ya ijumaa tarehe 19/10/2012 hii ni mara ya pili mwaka huu kwa Mheshimiwa Gama kuchangia baada ya kuchangia mwezi juni 2012 wakati wa maadhimisho ya siku ya wachangia damu duniani ambayo kitaifa yalifanyika mkoani hapo.
No comments: