Saturday, October 13, 2012

VURUGU ZA KIDINI ZAINGIA TANZANIA.(VIONGOZI WA NCHI WANACHOCHEA)


Baadhi ya wafanya furugu wakipambana na polisi

Baadhi ya vizuizi vilivyowekwa na waandamanaji katika eneo la Mbagala Kizuiani katika harakati za kupinga kitabu kitakatifu cha Koran kukojolewa na mtoto Emmanuel Josephat. Picha na Happy Mnale

Mojawapo ya makanisa yanayosemekana kuharibiwa likiungua moto


Vurugu zilizofuatia mtoto anayeitwa Emanuel Josephat(14)’ kukojolea msaafu (Quran) zimechukua sura mpya baada ya baadhi ya waumini wa dini ya kiislam kukusanyika na kushinikiza mtoto huyo aachiwe na polisi ili wamuue.


Waumini hao wanaokadiriwa kufikia idadi ya watu 3000 baada ya kutawanywa na Polisi waliingia mitaani na kuchoma moto kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania(KKKT), Mbagala Zakhem, wakaharibu Kanisa la Anglican, wakavunja vioo vya kanisa la Wasabato, na kuchoma moto Tanzania Assembly of God (TAG), la Mbagala Kizuiani na kuchukua vifaa vya muziki vya kanisa hilo na kuvichoma moto hadharani.


Awali waumini hao walikusanyika katika kituo hicho cha polisi cha Maturubai, Mbagala Kizuiani wakitaka mtoto huyo ambaye alikuwa chini ya ulinzi wa polisi aachiwe na Polisi walipokataa matakwa yao ndipo vurugu hizo zilipoanza.

Chanzo cha tukio hili ni mabishano baina ya watoto wawili, Emmanuel Josephat, na mtoto mwingine wa Kiislam.

Watoto hao walikuwa wakibishana kuhusu imani na dini ambapo mtoto wa Kiislam alimwambia Emmanuel kuwa, “Quran ni kitabu kitakatifu, endapo utafanya chochote kibaya juu yake basi utadhurika, waweza kuwa kichaa”.

Hapo ndipo Emmanuel alipoamua kuikojolea Quran ili kuona kama atakuwa kichaa.

Vurugu hizo ambazo zimesababisha gari za polisi namba T142 AVV,PT 0966 na T 325 BQP,basi la uda na gari la waandishi wa habari kutoka Clouds zikiharibiwa kwa mawe na waandamanaji hao.

Kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) kilionekana kuzidiwa nguvu na watu hao ambao walikuwa wakiwatawanya kutoka eneo moja wanakimbilia eneo lingine na kuleta madhara mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufunga barabara.

Hatahivyo baada ya viongozi wa dini hiyo kufika wakiwa wameambatana na Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sheikh wa Taasisi na Jumuiya za Waislamu kukaa kikao na kamanda wa Polisi Wilaya ya Temeke, David Misime, walifikia muafaka wa kuwaita waislamu hao na kuwatuliza lakini hali iliendelea kuwa si shwari kwani baada ya viongozi hao kuona waandamanaji hao wakikamatwa na kupigwa walikuja juu na kutishia kuondoka.

“Ndio nini sasa sisi tupo hapa kwa kuleta suluhu lakini ili waislamu watulie lakini mnawapiga mbele yetu ndio nini sasa!?” alihoji mmoja wa viongozi hao

No comments: