Wednesday, October 24, 2012

NDEGE YA JWTZ YAPATA AJALI NA KUUA RUBANI MWANAFUNZI

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limempoteza rubani wake mwanafunzi Kapteni Deo Mangushi baada ya mwavuli wake wa kujiokolea kushindwa kufanyakazi.


Rubani mwenzake waliokuwa katika mafunzo Kapteni F Kwidika anatibiwa majeraha hospitali ya Lugalo.

Marubani hao waliokuwa mafunzoni walikuwa wanatumia ndege ya mafunzo.

Inaaminika kwamba walipoona hitilafu walibonyeza mfumo wa kujiokoa na kutupwa nje ya ndege wakiwa kwenye viti umbali wa meta 100 kwa kasi ya risasi.

Msemaji wa JWTZ, Kanali Kapambala Mgawe, alisema ajali hiyo ilitokea leo saa 4:25 asubuhi katika Kikosi cha Anga , Ukonga jijini Dar es Salaam.

Wakati ajali inatokea ilikuwa mita 100 kutoka usawa wa ardhi haikuelezwa kama kuna watu wengine waliathirika na ajali hiyo.

No comments: