Monday, October 1, 2012

MTANGAZAJI MSTAAFU-DEBORAH MWENDA


Mtangazaji wa redio Mstaafu mama Deborah Mwenda na Mumewe  John -Baptist Mwenda (kulia) wakifurahia picha ya familia ambayo wamo wajukuu wao. Walizawadiwa picha hii jijini Dar wakati wakiadhimisha sherehe ya Jubilei ya dhahabu ya miaka ya ndoa. Zawadi hii ilikabidhiwa na mjukuu wao Vusile Terence (Kushoto) kwa niaba ya wanafamilia na wajukuu.
Kwa wale vijana wa miaka ya 80 watakuwa wanakikumbuka kipindi kile cha RTD siku ya jumamosi saa nane  mchana cha mama na mwana. Mimi binafsi nilikuwa sichezi mbali na redio wakati huo nikiwa nasikiliza hadithi pendwa  za mama/bibi  huyu kama zile za Adili na Nduguza, Binti Chura, Babu Zimwi na nyinginezo. Mama/bibi  huyu ni hazina kubwa kwa vizazi vya sasa na vijavyo katika tasnia ya habari.


(Picha naMohamed Mambo/DailyNews Tanzania kupitia  Wavuti)

No comments: