Wednesday, October 3, 2012

AJALI MBAYA YATOKEA MBEYA


Mbunge wa viti maalum Dr Mary Mwanjelwa akiwa katika hospitali ya Ifisi mara baada ya ajali.


Watu zaidi ya nane wamekufa baada ya lori la mafuta kufeli breki na kuyagonga magari mengine matatu katika mtelemko wa mlima wa Iwambi – Mbalizi nje kidogo ya Jiji la Mbeya.


Katika ajali hiyoiliyotokea majira ya saa nane mchana, Mbunge wa viti Maalum CCM Mkoa wa Mbeya, Mary Mwanjelwa alinusurika kufa baada ya gari alilokuwa akisafiria, kugongwa na kuteketea kabisa kwa moto na kusababisha kifo cha Katibu wake, ambapo mbunge huyo amelazwa katika Hospitali Teule ya Ifisi

Baadhi ya watu waliioshuhudia ajali hiyo, walisema kuwa lori hilo la mafuta lilifeli breki na kuanza kutelemka kwa kasi katika mlima huo, ambapo liliyagonga magari matatu ukiwamo Hiace yenye namba za usajili T 587 AHT.

Kwa upande wake, Muuguzi wa Hospitali ya Ifisi, Sikitu Mbilinyi alisema mbunge Mwanjelwa analalamika zaidi maumivu katika sehemu ya mgongoni na miguu sawa na dereva wake ambaye naye analalamikia miguu na amepasuka sehemu ya kichwani.

PICHA NA HABARI : MBEYA YETU BLOG

No comments: