Monday, September 3, 2012

TAHRIRI YA FATHER KIDEVU AKIMLILIA MWANGOSINa Mroki Mroki,

Nadhani hakuna Mtanzania aliyesoma walau shule ya Kata ana hajui kazi za Polisi wa Tanzania, Kazi yao Kubwa ni Kulinda Raia na Mali zao pamoja na Kusimamia sheria za Nchi zinafuatwa.


Lakini kubwa kabisa hapa ni Ulinzi wa Raia na Mali zao.

Hilo tuliache maana sidhani kama linafanywa na kama lingekuwa linafanywa Yanini sasa pawepo na makampuni Binafsi ya Ulinzi. Ni Makampuni haya ni chanzo cha Raia kukosa imani na Chombo chenye Mamlaka ya Ulinzi wao.

Lakini Vipi waue? Ni hatua ipi inatakiwa ifikiwe kabla ya Kuua? Ni wakati gani askari anapaswa kuua? Na anaua mtu wa aina gani? Je ameuawa Mtuhumiwa wapi. Utapatikana Ushahidi juu ya kosa lake lililompa hukumu hiyo kubwa? Inamaana Polisi waliona Kosa la Hayati Daudi Mwangosi aliyekuwa akihoji kukamatwa kwa mwandishi mwingine Hukumu yake ni Kifo? Kama alistahili kufa, je kifo kile ndio sahihi cha kumlipua na Bomu hata familia yake ishindwe utazama mwili wakati wa kumhifadhi? Marekani ilimtuhumu Sadam Husein kwa makosa mbalimbali lakini kwanini walipomkamata hawakumuua hadi walipofika Mahakamani na Hukumu kutoka kuwa anastahili kufa kwa Kunyongwa tena Hadharani? Polisi wanasema raia wasichukue sheria mikononi lakini je wao walipewa na nani sheria ya kuua mtuhumiwa ambaye wanauwezo wa kumfunga pingu? Nijuavyo mimi kama Mwangosi alikuwa ni mtu hatari basi kwanini wasinge mvunja Mikono tu au miguu kasha ahojiwe baadae kwa kuhatarisha amani?

Alamsiki!

No comments: