Thursday, September 6, 2012

KIPINDI MAALUM CHA HAMZA KASSONGO -MAUAJI YA MWANGOSIKatika video hii, ungana na waliopo studioni, Jesse Kwayu, Mhariri Mtendaji wa gazeti la Nipashe (IPP Media), Irenei Kiria, Mkurugenzi Mtendaji wa Sikika na mwenyeji wao/wetu Hamza Kasongo.


Mada inayojadiliwa ni, "UHUSIANO KATI YA POLISI, RAIA NA VYAMA VYA SIASA" hasa kwa kuzingatia matukio yaliyopita ambapo raia walipoteza maisha katika rabsha zilizozuka baina ya Polisi na baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa (Arusha, Mara, Mwanza, Tabora, Singida Morogoro), na tukio la hivi karibuni ni la mwanahabari Daudi Mwangosi kilichotokea huko Iringa.
Mwangosi (mwenye Kamera) na  kamanda wa Polisi Iringa -Kamuhanda muda mchache kabla hawajautoa uhai wake
SHUKURANI za dhati zimwendee Khaleed Mohd ambaye ameweka video hii na nyingine kwenye mtandao wa youtube, video zenye habari na taarifa muhimu hasa kutoka kwenye kituo cha runinga cha Channel TEN.CHANZO: WAVUTINo comments: