Thursday, August 23, 2012

MAHOJIANO BAINA YA MKULIMA NA MWANDISHI
Mkulima amejiwa na Mwaandishi wa magazeti kumuhoji kuhusu maisha ya shambani. Mkulima huyu hawapendi Waandishi wa habari, akaona vyema amchoshe katika kujibu maswali, na mambo yakawa hivi:


MWANDISHI: Wewe unawalisha ng'ombe chakula gani?

MKULIMA: Ng'ombe yupi? Mweupe au Mwekundu?

MWANDISHI: Ng'ombe mweupe.

MKULIMA: Ninamlisha nyasi na viguta vya mahindi.

MWANDISHI: Na mwekundu?

MKULIMA: Vilevile nyasi na viguta vya mahindi.

MWANDISHI: ahaa sawa, na sehemu ya kulala ni wapi?

MKULIMA: Ng'ombe yupi? mweupe au mwekundu?

MWANDISHI: Mweupeee!!!!XXCCCZZZZHH!

MKULIMA: Mweupe ninamlaza bomani kulee...

MWANDISHI: na mwekundu?

MKULIMA: Vile vile namlaza na mwenzie.

MWANDISHI: Hii sehemu yote majumba mengi, wakati wa kulisha unafanyaje?

MKULIMA: Yupi? mweupe au mwekundu?

MWANDISHI: Woooteeee!!!! [akifuka kwa hasira]

MKULIMA: Mweupe ninamfunga kamba na kumzungusha malishoni na kumrudisha.

MWANDISHI: na mwekundu vilevile?

MKULIMA: Mwekundu? Mwekundu yeye namfunga kamba na kuzunguka nae kama mwenzie tu.

MWANDISHI: Kwanini kila mara nikikuuliza huduma za ng'ombe wako unaniuliza mweupe au mwekundu halafu inatokea kuwa kazi zao wote ni sawa?????

MKULIMA: Kwa sababu ng'ombe mweupe ni wangu.

MWANDISHI: na mwekundu?

MKULIMA: na mwekundu ni wangu vilevile.

shuwaini.


Shukran Dada Subi: Posti hii ni ya  Nov 22' 2009 katika ukurasa wangu wa  face book .

No comments: