Friday, July 20, 2012

TAHADHARI YA MATAPELI KWA WALIOKO DAR

I hope you are well.I am writing this email because of an incident that happened to my dear friend on 6th July 2012 at Mlimani City, Dar-es-salaam.TZ.


Mtu asiemjua alimsimamisha kwa kumuita kwa jina lake Mlimani city wakati amemaliza shopping (muda wa saa mbili kasoro usiku baada ya kutoka kazini). Yule kaka akajaribu kumkumbusha matukio mbalimbali ya huko nyuma (kama mtu anayemfahamu).


Anasema alisogea restaurant kununua maji na hilo ndio tukio la mwisho analolikumbuka. Saa saba usiku amerudishwa nyumbani kwake na gari yake akiwa bado hana fahamu. Wamemchukulia simu, hela na baadhi ya hela zimetolewa kwenye ATM machines.


Thank God hawakudhuru kabisa. Ila kinachoogopesha ni kwamba huyu mtu alikuwa anajua historia yake (ndugu zake na marafiki zake) na anajua anapoishi. It is very disturbing.


Naomba mufahamishe ndugu na marafiki zenu kuhusu tukio hili. Ubinaadamu haupo tena kwahivyo tuwe makini tukiwa tunatembea huko mitaani...I hope this email will help others to avoid such tragedies!!STYLE YA PILI


Kutoka kwa Mdau Andrew

Kuna utapeli wa aina nyingi sana hasa parking ya Mlimani City! Wenye magari kuweni makini sana! Juzi naingia kwa gari naondoka jamaa akanifuata ati anataka msaada nikamwona mapema kabisa anavyobadilisha sura ili aoenekana mhitaji msaada!


Nikamuwahi nikafunga vioo! Nikashusha kidogo nikamhoji akadai ati anaomba japo nauli arudi gerezani! (Just imagine the way he confused himself kwani nilimchenjia ni balaa) Sasa gerezani umetorokaje, kwanza huna uniform, then umefanikiwa kutoroka bado unataka urudi, LOL!


Nilipotafakari na kumsimulia jamaa yangu akadai ndiyo janja yao, anakuomba msaada na ukishampatia anakushukuru kwa kukupa mkono, hapo ndipo inakuwa imekula kwako kwani wana kitu cha nja kali kama kisindano kidogo wanakuchoma nacho mnapopeana mkono then from there unapoteza fahamu, na ndipo wenzake wanatokea.


Unapakiwa kwa gari wakidai ndugu yao kazidiwa, unapelekwa kusikojulikana, wazee wanasepa na gari! BEWARE tupunguze ukarimu waTZ, wema usizidi uwezo!


tuwe makini jamani....

No comments: