Tuesday, June 12, 2012

MIRADI YA SH. 140 MILIONI YAZINDULIWA LINDI
Mwanja Ibadi, LindiMIRADI 10 yenye thamani ya Sh138 milioni imezinduliwa wilayani Lindi katika mbio za mwenge mwaka huu.Miradi hiyo ni ya maji, vyoo, madarasa, zahanati, ujenzi wa nyumba za walimu, majengo ya utawala na miradi mbalimbali ya kilimo ambayo iko katika hatua za kukagua, maweka mawe ya msingi na kufungua.


Hayo yalielezwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Hijob Shankalwa wakati akisoma risala kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Ali Hamidi kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge, Honest Mwanosa.


Shamkalwah alisema Sh29 miliomni kati ya fedha hizo, zimenunulia kivuko, Sh900,000 zimeanzisha kitalu cha mihogo, Sh350 zimejenga ofisi ya wapinga rushwa na Sh28 milioni zimetumika kwa ujenzi wa madarasa.


Alisema utekelezaji wa miradi hiyo umefanikiwa kutokana na ushirikiano baina ya wananchi wa wilaya hiyo na serikali yao.


Naye Mwanosa aliwataka wananchi wa wilaya hiyo kuendeleza umoja na mshikamano uliosisiwa na Baba wa Taifa, mwalimu Julius Nyerere, ili kudumisha amani na utulivu wa nchi.


Aliwataka wananchi wa Mkoa wa Lindi kuwapuuza viongozi wa siasa wanaohamasisha maandamano na vurugu kwa kuwa hawana nia mzuri na wananchi, bali wanalenga kuvuruga amani na utulivu wa Watanzania.


Kiongozi huyo wa mbio za mwenge aliwataka vijana na jamii kwa ujumla kuacha kukata tamaa na kuendelea kukaa vijiweni, badala yake wafanye kazi kwa juhudi, ili kuondokana na umaskini, ujinga na maradhi, bila kusahau kupiga vita uushwa na Ukimwi.


Ujumbe wa mbio za mwenge mwaka huu ni ‘Sensa ni msingi wa mipango ya maendeleo yetu, mwananchi shiriki kuhesabiwa Agosti 26, mwaka huu; na mabadiliko ya Katiba shiriki kutoa maoni yako’.
MWANANCHI

No comments: