Wednesday, June 20, 2012

MAADHIMISHO YA SIKU YA WACHANGIA DAMU NA UFUNGUZI WA KITUO KIDOGO CHA DAMU SALAMA LINDI YAFANA

Mkuu wa Mkoa Mh Ludovick Mwananzila akisoma hotuba yake kwa wananchi wa Lindi waliohudhuria maadhimisho ya siku ya wachangia damu duniani yaliyoambatana na ufunguzi wa kituo kidogo cha damu salama mkoani Lindi
Mgeni Rasmi Mkuu wa Lindi Mh Ludovick Mwananzila akikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo kidogo cha damu salama mkoani Lindi
Mgeni Rasmi akielekezwa mawili matatu na meneja wa Mpango wa Damu Salama Kanda ya Kusini Dr. Vincent Mtweve wakati wa ufunguzi wa kituo kidogo cha damu salama mkoa wa Lindi
Mkuu wa Mkoa akijadiliana na watendaji mbalimbali wa mkoa wa Lindi wakati wa uzinduzi wa kituo kidogo cha damu salama
Wadau wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama. Kutoka Kushoto ni Mdau Gustav Kinongo ambaye ni msimamizi mkuu wa masuala ya fedha na Meneja Wa Mpango wa taifa wa damu salama kanda ya kusini Dr. Mtweve
Wanafunzi mbalimbali wa shule za jirani na manispaa ya Lindi hawakuwa nyuma katika kushiriki kwao na kwa kiasi kikubwa wao ndio wadau na wachangiaji wakubwa wa damu . Shukrani kwa Wakuu wa Shule kwa kuweza kutoa ushirikiano katika maadhimisho ya siku ya wachangia damu duniani

No comments: