Thursday, June 28, 2012

HOTELI YA KIGOGO MMOJA SERIKALINI

Hili jengo lililopo maeneo ya Shangani Mtwara (jirani na VETA) kama bango lake la ujenzi linavyoelezwa kwamba litakapokamilika litakuwa hoteli ya kifahari mkoani Mtwara. Kumekuwa na minong'ono mingi kuhusu mmiliki halisi wa jengo hili ambapo asilimia kubwa ya watu wananong'oona kwamba mmiliki wake ni kigogo wa mambo ya nje mwenye ndoto ya kuwania Urais 2015 endapo ataoteshwa ndoto na Mungu.

Kuwekeza sio kitu kibaya ikiwa fedha imepatikana kwa njia ya halali na sio kwa kuwakandamiza walalahoi ili uwe mlalahai. Hata hivyo Blogu hii haina uthibitisho rasmi kama yeye ndio mmiliki halali wa jengo hili hata hivyo wahenga husema "Lisemwalo lipo kama halipo laja......"

No comments: