Thursday, June 21, 2012

HARAKATI ZA KUMTOA SHETANI ZAMWUA DIWANI

Watu wawili ambao ni Maustadhi wamedaiwa kumpiga Diwani wa Kata ya Stesheni wilayani Nachingwea mkoani Lindi, Saida Kaisi (41) ili kumtoa mashetani, na kusababisha kifo chake.

Kamanda wa Polisi mkoani Lindi, Kamishna Msaidizi George Mwakajinga amesema diwani huyo alienda kwa Maustadhi hao; Fadhili Mohammedi (28) na Juma Ustadhi (39) tarehe 14 Juni 2012, saa 3, marehemu alipelekwa kama mgonjwa ili atolewe mashetani ndipo Maustadhi hao walianza kumtibu kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Alidai kuwa Diwani huyo alikuwa na matumaini kuwa angepona, lakini hali ilizidi kuwa mbaya na hatimaye alikwenda hosipitalini na baada ya kufika katika Hosipitali ya Wilaya ya Nachingwea, alipatiwa huduma na kwa bahati mabaya alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu.

Kamanda Mwakajinga alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa na Polisi kwa kusaidia uchunguzi juu ya kifo hicho

WAVUTI

No comments: