Thursday, May 10, 2012

WAKUU WAPYA WA WILAYA
RAIS JAKAYA KIKWETE amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya nchini kwa kuwateua wapya 70, kuwabakiza kazini 63, kuwastaafisha 51, na kuwabadilisha vituo vya kazibaadhi yao.

Akitangaza uteuzi huo mbele ya Wahariri wa vyombo vya habari, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisema kutokana na mabadiliko hayo, Wakuu wa wilaya 51 kati ya 114 waliokuwepo zamani wameachwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ki-afya na umri mkubwa.

“Zamani tulikuwa na wilaya 114 na baada ya Mhe. Raisi Kikwete kuridhia kuanzishwa kwa wilaya mpya 19, hivi sasa zimefikia wilaya 133. Kwa hiyo, tumebakiza Wakuu wa Wilaya 63 na ukiongeza hawa wapya 70 unapata jumla yao ni 133,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu alisema miongoni mwa wakuu hao wapya wa wilaya, wengi wao ni vijana wenye umri kati ya miaka 30 hadi 45 na kwamba idadi yao inafikia 40. Alisema vilevile, idadi ya wakuu wa wilaya wanawake ni 43 sawa na asilimia 32.3.

Alisema wakuu wa wilaya watano kati ya 70 wapya walioteuliwa, wametokana na wabunge wa

viti maalum. “Lengo letu ni kutaka kuandaa viongozi wapya wa baadaye kutokana na kundi hili,” alisema.

Alisema Wakuu hao wapya wanatakiwa kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi ili waapishwe na Wakuu wa Mikoa husika na kisha watatakiwa kuhudhuria mafunzo maalum ambayo yatafanyika Dodoma. “Tumeandaa mafunzo hayo maalumu kwa ajili ya Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Makatibu Tawala wa Mikoa… siyo semina bali ni mafunzo na itabidi wapewe mitihani,” alifafanua.

Orodha kamili ya wakuu wa wilaya wapya na vituo vya kazi ni kama ifuatavyo:

NA. JINA KITUO CHA KAZI

1. Novatus Makunga -Hai

2. Mboni M. Mgaza- Mkinga

3. Hanifa M. Selungu -Sikonge

4. Christine S. Mndeme -Hanang

5. Shaibu I. Ndemanga- Mwanga

6. Chrispin T. Meela -Rungwe

7. Dr. Nasoro Ali Hamidi- Lindi

8. Farida S. Mgomi -Masasi

9. Jeremba D. Munasa- Arumeru

10. Majid Hemed Mwanga- Lushoto

11 Mrisho Gambo -Korogwe

12. Elias C. J. Tarimo -Kilosa

13. Alfred E. Msovella- Kiteto

14. Dkt. Leticia M. Warioba- Iringa

15. Dkt. Michael Yunia Kadeghe -Mbozi

16. Mrs. Karen Yunus -Sengerema

17. Hassan E. Masala -Kilombero

18. Bituni A. Msangi -Nzega

19. Ephraem Mfingi Mmbaga -Liwale

20. Antony J. Mtaka -Mvomero

21. Herman Clement Kapufi- Same

22. Magareth Esther Malenga -Kyela

23. Chande Bakari Nalicho -Tunduru

24. Fatuma H. Toufiq -Manyoni

25. Seleman Liwowa -Kilindi

26. Josephine R. Matiro -Makete

27. Gerald J. Guninita - Kilolo

28. Senyi S. Ngaga -Mbinga

29. Mary Tesha Ukerewe

30. Rodrick Mpogolo -Chato

31. Christopher Magala -Newala

32. Paza T. Mwamlima -Mpanda

33. Richard Mbeho -Biharamulo

34. Jacqueline Liana- Magu

35. Joshua Mirumbe- Bunda

36. Constantine J. Kanyasu- Ngara

37. Yahya E. Nawanda -Iramba

38. Ulega H. Abadallah -Kilwa

39. Paul Mzindakaya- Busega (mpya)

40. Festo Kiswaga -Nanyumbu

41. Wilman Kapenjama Ndile - Mtwara

42. Joseph Joseph Mkirikiti -Songea

43. Ponsiano Nyami -Tandahimba

44. Elibariki Immanuel Kingu -Kisarawe

45. Suleiman O. Kumchaya- Tabora

46. Dkt. Charles O. F. Mlingwa -Siha

47. Manju Msambya- Ikungi (mpya)

48. Omar S. Kwaangw’ -Kondoa

49. Venance M. Mwamoto -Kibondo

50. Benson Mpesya- Kahama

51. Daudi Felix Ntibenda -Karatu

52. Ramadhani A. Maneno- Kigoma

53. Sauda S. Mtondoo -Rufiji

54. Gulamhusein Kifu -Mbarali

55. Esterina Kilasi -Wanging’ombe (mpya)

56. Subira Mgalu -Muheza

57. Martha Umbula- Kongwa

58. Rosemary Kirigini- Meatu

59. Agness Hokororo- Ruangwa

60. Regina Chonjo -Nachingwea

61. Ahmed R. Kipozi - Bagamoyo

62. Wilson Elisha Nkhambaku - Kishapu

63. Amani K. Mwenegoha - Bukombe

64. Hafsa M. Mtasiwa - Pangani

65. Rosemary Staki Senyamule - Ileje

66. Selemani Mzee Selemani - Kwimba

67. Lt. Col. Ngemela E. Lubinga - Mlele (mpya)

68. Iddi Kimanta Nkasi

69. Muhingo Rweyemamu - Handeni

70. Lucy Mayenga - Uyui

Kuhusu Wakuu wa Wilaya wa zamani 63, Waziri Mkuu aliwataja waliobakishwa kazini na vituo vyao vya kazi kama ifuatavyo:

NA. JINA KITUO CHA KAZI

1. James K. O. Millya -Longido

2. Mathew S. Sedoyeka- Sumbawanga

3. Fatuma L. Kimario- Igunga

4. Capt. (Mst.) James C. Yamungu -Serengeti

5. Lt. (Mst.) Abdallah A. Kihato -Maswa

6. Sarah Dumba -Njombe

7. Jowika W. Kasunga -Monduli

8. Elizabeth C. Mkwasa- Bahi

9. Col. Issa E. Njiku -Misenyi

10. John B. Henjewele- Tarime

11. Elias W. Lali -Ngorongoro

12. Raymond H. Mushi- Ilala

13. Francis Miti -Ulanga

14. Evarista N. Kalalu -Mufindi

15. Mariam S. Lugaila- Misungwi

16. Anna J. Magowa -Urambo

17. Anatory K. Choya -Mbulu

18. Fatma Salum Ally -Chamwino

19. Deodatus L. Kinawiro- Chunya

20. Ibrahim W. Marwa -Nyang’hwale (mpya)

21. Dkt. Norman A. Sigalla- Mbeya

22. Moshi M. Chang’a -Mkalama (mpya)

23. Jordan M. Rugimbana -Kinondoni

24. Georgina E. Bundala -Itilima (mpya)

25. Halima M. Kihemba- Kibaha

26. Manzie O. Mangochie- Geita

27. Abdula S. Lutavi -Namtumbo

28. Zipporah L. Pangani -Bukoba

29. Dkt. Ibrahim H. Msengi- Moshi

30. Col. Cosmas Kayombo -Kakonko (mpya)

31. Lembris M. Kipuyo -Muleba

32. Elinasi A. Pallangyo- Rombo

33. Queen M. Mlozi -Singida

34. Juma S. Madaha -Ludewa

35. Angelina Mabula -Butiama (mpya)

36. Hadija H. Nyembo- Uvinza (mpya)

37. Ernest N. Kahindi -Nyasa (mpya)

38. Peter T. Kiroya -Simanjiro

39. John V. K. Mongella -Arusha

40. Baraka M. Konisaga -Nyamagana

41. Husna Mwilima -Mbogwe (mpya)

42. Sophia E. Mjema -Temeke

43. Francis Isaac -Chemba (mpya)

44. Abihudi M. Saideya -Momba (mpya)

45. Khalid J. Mandia -Babati

46. Anna Rose Nyamubi- Shinyanga

47. Dani B. Makanga- Kasulu

48. Amina J. Masenza -Ilemela

49. Mercy E. Silla -Mkuranga

50. Christopher R. Kangoye -Mpwapwa

51. Lt. Edward O. Lenga -Kalambo (mpya)

52. Halima O. Dendego- Tanga

53. Lephy B. Gembe -Dodoma

54. Saidi A. Amanzi -Morogoro

55. Jackson W. Msome- Musoma

56. Elias C. B. Goroi- Rorya

57. Lt. Col. Benedict Kitenga- Kyerwa (mpya)

58. Erasto Sima- Bariadi

59. Nurdin H. Babu- Mafia

60. Khanifa M. Karamagi -Gairo (mpya)

61. Gishuli M. Charles -Buhigwe (mpya)

62. Saveli M. Maketta- Kaliua (mpya)

63. Darry Rwegasira -Karagwe

(mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 3021,

DAR ES SALAAM.

JUMATANO, MEI 9, 2012.

No comments: