Tuesday, May 8, 2012

MAMA AUZA KICHANGA ILI ANUNUE TUKU TUKU .

Msichana Imaculata Joseph (19) amesema, amemuuza mtoto wake mchanga wa kike mwenye umri wa miezi miwili.

Binti huyo mkazi wa eneo la Majengo Mtaa wa Gezaulole mkoani Mtwara, amewaeleza Polisi kuwa amekiuza kichanga hicho kwa bei ya milioni 1.5/-, na kwamba, ametumia fedha hizo kununua pikipiki kwa ajili ya biashara.

Hata hivyo bado kuna utata kuhusu sakata hilo kwa kuwa msichana huyo anayedaiwa kuwa mlevi wa pombe za kienyeji, pia amesema kuwa amemuuza mwanawe kwa shilingi lakini mbili.

Utata kuhusu kutoweka kwa mtoto huyo umezidi kuongezeka kwa kuwa, inadaiwa kuwa, msichana huyo alikaririwa akisema kilabuni kuwa, anataka kumuuza mwanawe, na siku chache baadaye, kichanga hicho hakikuonekana tena, na mama huyo akadai kuwa mwanawe kaibwa.

Ofisa Mtendaji wa eneo analoishi msichana huyo, Yusuf Mfaume amethibitisha kutoweka kwa kichanga hicho kilichotimiza umri wa miezi miwili Aprili 25 mwaka huu.

Mfaume amesema, taarifa kuhusu kupotea kwa kichanga hicho zinachanganya, na kwamba, msichana huyo ni mwenyeji wa kijiji cha Lulindi wilayani Masasi.

Inadaiwa kuwa, Imaculata amemuuza mwanawe huyo kwa mwanamke anayetoka Morogoro.

Kwa mujibu wa Mfaume, msichana huyo ni mlevi, na kwamba, hata yeye alizungumza naye baada ya kumnunulia pombe za kienyeji. Polisi wamemuachia binti huyo kwa dhamana, uchunguzi unaendelea.


No comments: