Tuesday, April 10, 2012

MJADALA MAALUM: UMEFIKA WAKATI SASA WA HALMASHAURI /MANISPAA KUWA NA E.M.S NA FIRE BRIGADE YAKE
Na M.M Mwanakijiji,


Wakati umefika wa kuondoa Idara ya Uokoaji kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na kufanya jukumu hilo kuwa ni suala la Halmashauri na Manispaa nchini. Kwa muda mrefu - naamini tangu uhuru - huduma ya uokoaji (rescue service) imekuwa ni sehemu ya wizara ya mambo ya ndani na kufuata mfumo wa kijeshi ambao uko Polisi na Magereza. Sheria ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji ya mwaka 1985 imetengeneza kikosi cha taifa zima.

Kutokana na Sheria hii kikosi kizima kinasimamiwa na Kamishna ambaye anateuliwa na Rais na hivyo kufanya watendaji wake wasiwajibike moja kwa moja kwa halmshauri na miji ambayo wanatumikia; mishahara yao inalipwa toka hazina na wanawajibika kwa uongozi wa kisiasa wa taifa zaidi. Sheria pia inamuweka Kamishna chini ya Waziri ambaye pamoja na kusimamia Jeshi la Polisi pia anasimamia Uhamiaji, Magereza na Wakimbizi.


Kwa ufupi, jeshi hili limekuwa centralized bila ya sababu kubwa hasa katika kipindi hiki ambacho miji yetu inakua kwa kasi na watu wetu wanatawanyika zaidi na zaidi. Ni muhimu kulifanya jeshi au kikosi hiki kuwa cha mahali zaidi na kukifanya kiwajibike kwa mahali kilipo; kwa mfano kichukue amri yake kutoka kwa Meya wa mahali (siyo mkuu wa mkoa au wilaya). Kiundwe ili kiweze kuajiri na kusimamia mambo yake; kila mji uwe na kikosi chake.


Lakini siyo kwenye suala la "fire brigade" tu lakini kwenye mji mkubwa kama wa Dar-es-Salaam halsmahauru zinahitaji kuwa na Idara zake za Huduma ya Tiba ya Dharura (Emergency Medical Service) ambayo itawajibika kuitikia wito wa matatizo ya tiba. Mifano iko mingi na ya kutosha ya watu kukosa huduma nzuri ya kwanza kwa haraka kwa sababu ama hakuna magari, hakuna huduma hiyo au mahali ilipo ni huduma ambayo ni binafsi sana na haiwajibiki kwa wananchi. Inawezekana kabisa kuwa na huduma moja ya uokoaji na medical rescue au vikawa vitengo viwili tofauti ndani ya mji mmoja.


Nini kifanyike:


a. Mabadiliko ya Sheria ya Kikosi cha Zimamoto na Ukoaji ili kuruhusu na kulazimisha halmshauri ya mjini nchini kuwa na kugharimia kikosi chake cha uokoaji na huduma ya tiba ya dharura. Sheria mpya itaachilia kila halmshauri kujiundia mfumo wake wa uokoaji chni ya viwango vitakavyokuwa vimewekwa kitaifa.


b. Vikosi vyote vya sasa vya uokoaji kuingiziwa katika ajira za halmashauri, mali na vitu vyao kuingizwa huko. Lakini hili pia litatengeneza uwezekano wa kutengenezwa ajira mpya kwenye halmshauri mbalimbali ambazo kwa sasa hazina huduma hiyo au zinategemea huduma kutoka mikoani au taasisi binafsi. Hili la uokoaji na huduma ya afya ni lazima lionekane ni haki ya wananchi kama vile huduma ya polisi.


c. Nafasi za ajira mpya kwa vikosi hivi ziende kwa maafisa wa polisi abmao wangependa kutoka kwenye upolisi na kwenda kwenye uokoaji. Hili liendane na kufanya maafisa wa Uokoaji wawe na nguvu za kipolisi vile vile. Sidhani kama sheria ya sasa hivi inawapa nguvu za kutosha za kipolisi.


d. Mabadiliko haya yatapunguza mzigo wa kuendesha jeshi hili kitaifa kwenye bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani; na badala yake mzigo huu utaenda kwenye halmashauri ambazo zitatakiwa kupanga bajeti yake kwa kuanglaia mahitaji yake. Kwa mfano, mji wa Hanang kwa mfano unaweza usiwe na mahitjai sawa na Kinondoni lakini bado ni mahitaji. Kwa hiyo Hanang wanaweza kuajiri maafisa 10 tu wakati Halamshauri ya Kinondoni ikajikuta inahitaji maafisa 200.


e. Maisha ya wananchi wetu yataanza kuokolewa kwa haraka zaidi kutokana na kupatikana kwa huduma ambayo inawajibika kwao. Leo hii watu wanahangaikaa kukimbiza wagonjwa hospitali kwa sababu hawajui wakipiga simu ya "emergency" yule anayejibu atafanya nini. Miji kama Dar ikipewa uwezo wake inaweza hata kununua Med-Vac Helicopters yaani chopa zinazotumika kuwahi watu walio katika matatizo ya hatari ya afya ambao kuwasafirisha kwa barabara itakuwa ni kupoteza muda zaidi.


f. Hospitali kama Muhimbili na hospitali nyingine kubwa zianze kufikiria kujenga au kuwa na maeneo ya kufikishia wagonjwa kwa njia ya helikopta; yaani kujenga Heliports..


Na mambo mengine yanawezekana kufanya hivi. Hili halihitaji fedha kutoka serikali kuu bali kutoka kwenye halmashauri. Halmashauri ambazo hazina uwezo sana zinaweza kupair up na halmashauri nyingine na maeneo ambayo ni madogo sana ndio yanaweza kuhudumiwa ama na sekta binafsi kwa mkataba au na vikosi vya polisi ambavyo vina mafunzo hayo zaidi chini ya serikali kuu.


Hili lawezekana au haliwezekani na kwanini?E.M.S -Maana yake ni Emergency Medical Services.
JAMII FORUMS

No comments: