Thursday, April 5, 2012

JIMBO LA ARUSHA MJINI LAPOTEZA MBUNGE WAKE KWA MUDA.


Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kupitia CHADEMA, amepoteza kiti hicho kwa kuenguliwa na Mahakama katika kesi iliyokuwa inamkabili ya kupinga ubunge wake.

Kesi hiyo iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga (55), Happy Kivuyo (49) na Agnes Mollel (44) ambao walikuwa wanamtuhumu Mbunge huyo kwa kutoa kauli za udhalilishaji, matusi na kashifa kwa aliyekuwa mgombea wa Ubunge jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Dkt. Batilda Buriani.

Hukumu hiyo iliyosomwa na Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Sumbawanga, Gabriel Rwakibarila.

Katika hukumu hiyo, Lema hakuondolewa haki ya kugombea ubunge huo kwa kuwa kosa lililomtia hatiani ni matumizi mabaya ya lugha tofauti na ilivyodhaniwa kuwa ni vitendo vya rushwa. Uamuzi wa kugombea ama kutokugombea kiti hicho tena utatokana na maamuzi yake mwenyewe na ridhaa ya chama chake ikiwa kitamteua na kumpitisha kugombea.

Taarifa za watu wa karibu zinasema kuwa Lema hatakata rufaa mahakamani juu ya hukumu ya kesi hiyo, bali atakata rufaa kupitia kura ya wananchi wa Arusha Mjini wakati wa kugombea kiti hicho.

Hivyo tutarajie uchaguzi mpya ndani ya siku 90. Tanzania, nchi ya uchaguzi kila uchao...!

Kweli tunahitaji Katiba Mpya yenye kukidhi haja na inayoendana na wakati.

CHANZO: WAVUTI

No comments: