Monday, April 16, 2012

HERI KWA SIKU YA KUZALIWA KAMANDANa Ridhwan Kikwete,

Amani ya bwana iwe nasi sote.

Waungwa waliwahi twambia kuwa ...'hakuna
mwalimu mzuri zaidi ya yale ambayo wengine wamepitia"". maneno haya ni mazito kwa upande mmoja lakini ni mwalimu wa ukweli kwa maana yake.

Katika safari ya maisha yangu ni mengi nimekutana nayo na mengine kusimuliwa. Nimeona watu walivyo na roho ndogo na tamaa , nimeona watu wakisalitiana na hata pia kumsaliti mungu , na nimeona pia mazuri, mafanikio na hata furaha katika mioyo ya watu. binafsi nimeyashiriki hayo. mungu awape moyo mwepesi na wa kutambua wote ambao katika macho yake , wameharibikiwa na awapunguze katika mitihani inayowakaribiri ya mazuri ya ulimwengu huu.

Leo hii ni siku nzuri kwangu kwa kuwa ni siku yangu ya KUZALIWA. Binafsi ni furaha sana kutokana na uwepo wenu nyinyi ambao kwa lugha moja , nawatambua kama wasomi wa tafakuri hii. kwa upande mwengine ni mapenzi ambayo naendelea kupata toka kwa wazazi wangu,wadogo zangu na ndugu zangu wote.Pamoja na hayo, mapenzi matamu toka kwa mke wangu na watoto wetu wawili ambao ni wewe baba mungu ambaye umetujalia kupata.

Siku hii pia imepata tatizo pia. kwanza , nashereheka huku nikiwa na pengo kubwa la kupoteza rafiki yangu, bwana Kanumba ambaye kwa pamoja tulidhamiria kurejesha mapenzi ya kweli kwa ndg ambao kwa tafsiri wamepotea. nazungumzia mahusiano mabaya au mpasuko ulioanza katika tasnia ya cinema za kiswahili BONGOMOVIE .mungu akulaze pema , unapostahili rafiki yangu.

Lakini kwa upekee, ni kupoteza kijana James Millya aliyekuwa Mwenyekiti wa Vijana wa mkoa wa Arusha. kwangu mimi ninamtakia kila la kheri katika makazi mapya. ninampongeza tena kwa kufanya maamuzi ambayo hata kama atakuja kujutia baadae ni kwa kuwa amefanya maamuzi ambayo sidhani kama atakuwa amemshirikisha mtu japo kwamba yapo maneno kuwa wako wakubwa na marafiki wake wa karibu ambao amewashirikisha. Tabu kwangu inakuja kama kuna mtu ndani ya chadema ambaye amewahi mshirikisha , japo nijuavyo mimi haiwezi kuwa hadithi ya kuokota embe kwenye mbuyu.hii inanipa alama nyengine ya sehemu ya kumbukumbu ndani ya siku hii adhimu katika maisha yangu.itabaki kuwa na upekee kwa kuwa kila ninaposherehekea siku hii nitakukumbuka.

Mwisho, kabisa, niendelee kukutakia kheri kiongozi wa Kanisa la Wakatoliki duniani,Pope Benedict xvi, ambae kwa pamoja nami tunasherehekea siku hii muhimu maishani mwetu. najua na natambua kuwa siku hii ina umuhimu wa kipekee. Katika maombi na sala zako. tuombee nasi tuliohuku kusini mwa jangwa la sahara, umri mrefu na mafanikio kama uliyonayo wewe. Ukiwa kama alama ya upekee katika uongozi wa watu wake, mungu akupe hekima na muongozo ili uwe mwenye kutenda haki na haki hiyo ionekane. AMIN

mwisho, niendelee kuwashukuru wote washabiki wangu, marafiki zangu toka mtaanighetto, kwenye makambi balimbali, wasomi, wanafunzi, masokoni, kwenye mitandao ya kijamii Twitter,Facebook na kadhalika na wote ambao tunasimama kuhakikisha haki inatendeka katika wakati muafaka na pasi kuruhusu wanyonge waendelee kuonewa na wachache wanaojiona kuwa wao ndiyo wenye maono ya ukweli angali wamesahau kuwa ni wapofu wasioona hata kama viatu vyao viko na vumbi; niwatakie kheri na baraka tele katika siku hii muhimu kwangu.

aksanteni sana.

Kutoka kwenye Facebook page yake

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana kwa siku ya kuzaliwa.