Thursday, March 22, 2012

UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: UTEUZI

NA UHAMISHO WA MAKATIBU TAWALA WA MIKOARais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho

Kikwete, leo, Jumatano, Machi 21, 2012 ameteua Makatibu Tawala wa
Mikoa saba na kufanya uhamisho wa wengine watatu.Ifuatayo chini ni
taarifa kamili iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y.
Sefue ikitangaza uteuzi huo:-

A: MAKATIBU TAWALA WA MIKOA


(i) Dkt. Faisal Hassan Haji ISSA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa

Mkoa wa KILIMANJARO. Kabla ya hapo Dkt. Faisal alikuwa Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Rasilimali Watu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma.

(ii) Bibi Mariam Amri MTUNGUJA, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa

wa MBEYA. Kabla ya hapo Bibi Mtunguja alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.

(iii) Bwana Eliya Mtinangi NTANDU, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa

Mkoa wa MOROGORO. Kabla ya hapo Bwana Ntandu alikuwaKatibu Tawala
Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Dar es Salaam.

(iv) Bwana Severine Bimbona Marco KAHITWA, ameteuliwa kuwa Katibu

Tawala wa Mkoa wa GEITA. Kabla ya hapo Bwana Kahitwa alikuwa
Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Uchambuzi wa Sera, Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Dodoma.

(v) Eng. Emmanuel N.M. KALOBELO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa

wa KATAVI. Kabla ya hapo Eng. Kalobelo alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmasharui ya Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi.

(vi) Bwana Hassan Mpapi BENDEYEKO, ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa

Mkoa wa RUVUMA. Kabla ya hapo Bwana Bendeyeko alikuwa Kaimu Katibu
Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro.

(vii) Dkt. Anselem Herbert Shauri TARIMO, ameteuliwa kuwa Katibu

Tawala wa Mkoa wa SHINYANGA. Kabla ya hapo Dkt. Tarimo alikuwa Kaimu
Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma.Uteuzi huu unaanzia tarehe 21 Machi,
2012. Wataapishwa Ikulu, Jumamosi tarehe 24 Machi, 2012 saa nne
asubuhi.
B: UHAMISHO

(i) Bibi Mgeni BARUANI – Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro

anahamishiwa Mkoa wa NJOMBE.

(ii) Bibi Mwamvua A. JILUMBI – Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga

anahamishiwa Mkoa wa SIMIYU.

(iii) Bibi Bertha O. SWAI, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya anahamishiwa

Mkoa wa PWANI.

Balozi Ombeni Y. Sefue

KATIBU MKUU KIONGOZI

IKULU,

DAR ES SALAM.

21 Machi, 2012

No comments: