Thursday, March 8, 2012

MGOGORO WA SHULE YA SEKONDARI NDANDA WAHITIMISHWA RASMI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu bwana Selestine Gesimba akitoa taarifa kwa waaandishi wa habari juu ya makubaliano yaliyofikiwa baina ya Serikali na viongozi wawakilishi wa jumuiya ya kiislam juu ya mgogoro wa uongozi wa shule ya sekondari ya Ndanda na Wanafunzi. Mgogoro huo ulipelekea wanafunzi 62 kufutwa shule. Moja kati ya maazimio ya makubaliano hayo ni wanafunzi kurudishwa shuleni na kupewa fursa na haki ya kuabudu wawapo shuleni.
Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Ndanda waliosimamishwa masomo yao kutokana na mgogoro uliojitokeza baina yao na uongozi wa shule wakifuatilia kwa makini tamko la makubaliano baina ya viongozi wa dini ya Kiislamu lililotolewa kupitia mwakilishi wa Wizara ya Elimu bwana Selestine Gesimba


PICHA: MICHUZI

No comments: