Thursday, March 1, 2012

7 WAFA 12 WAJERUHI MWANZA

WATU wa saba wamefariki dunia baada ya magari mawili kati ya Basi lililokuwa likifanya safari zake toja jijini Mwanza kwenda wilayani Tarime kugongana na gari dogo la abiria Toyota Noha na kisha kupita juu ya hilo hivyo kusababisha abiria sita pamoja na dreva wake na majeruhi kuwa 12.

Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 3:13 asubuhi katika eneo Lugeye kata ya Nyanguge wilayani Magu, wakati basi la abiria Mali kampuni ya Zacharia aina ya Scania lenye namba za usajili T 655 BBP lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Wilayani Tarime kugongana uso kwa uso na Noha mali ya Ramadhani Kashakala wa Geita yenye namba za usajili T 716 BMV iliyokuwa ikitokea Magu mjini kuja Mwanza.

Hata hivyo kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza Liberatus Barlaw alisema kuwa waliofariki katika ajari hiyo ni watu watano huku abiria 11 waliokuwemo ndani ya basi hilo wakiwa wamejeruhiwa vibaya.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, ajali hiyo imetokea kutona na gari la Noha kuwa katika mwendo mkali huku yakifukuzana kuwahi abiri, ambapo wakati likijaribu kulipita Noha nyinge ilikutana na basi hilo na ndipo lilipogongwa na kusababisha vifo vya abiria watano waliokuwemo ndani yake.

“Ajali ilivyotokea, ni magari haya ya Noha yalikuwa yakifukuzana, sasa hii Noha iliyopata ajali ilipofika eneo hilo ikaanza kuipita nyingine, ikakutana na basi dreva wake alishindwa kurudi, ndipo wakagongana uso kwa uso, ile Noha nyingine ilipita” alieleza Jilala Tupa mmoja wa mashuhuda katika eneo la ajali.

Alisema akiwa katika usaidiaji ndani ya Noha waliweza kutoa Dreva aliytambulika kwa jina la Deus John (40) akiwa mzima ambapo kutokana na kuwa ameumia vibaya alikimbizwa Hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu na kwamba mbali na Dreva huyo waliweza kutoa miili ya watu wengine sita ambapo kati yao ilielezwa ku wote walikuwa abiria.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Muuguzi mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Bugando Egiupharasia Nyange amethibitishwa kupokea majeruhi watatu ambapo mmoja kati yao akiwa ni Dreva wa NOha ambaye alifariki muda mfupi wakati akihudumiwa.

“Hapa tumepokea majeruhi watatu, mwanamke mmoja na wanaume wawili mmoja ni dreva ambaye alifariki, majeruhi wengine hawakuwa na hali mbaya zaidi hivyo waliweza kuendelea na safari zao,” alieleza muuguzi huyo.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Barlaw, alisema kuwa marehemu wawili kati ya watano ndiyo waliofahamika kwa majina akiwemo dereva wa naoh hiyo Deus John (42) pamoja na abiria mmoja aliyefahamika kwa jina la Peter Lubisha (40).

Wakati huo huo jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu 19 ambao wanasadikika kuwa ni majambazi wa kutumia silaha za kivita.

Akitowa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari kamanda Barlaw alisema kuwa majambazi hayo yalikamatwa katika matukio tofauti tofauti wakiwa njiani kwa ajili ya kwenda kufanya uharifu.

Alisema katika matukio hayo jumla ya bunduki tatu za kivita aina ya SMG pamoja na risasi zake 65 zilikamatwa.

Akielezea tukio la kwanza Barlaw alisema kuwa mnamo februar 26 majira ya saa 4:30 usiku askali wakiwa doria walimkamata Jumanne Paskali (40) mkazi wa kigoma akiwa na bunduki namba BD 356690 na magazine moja na risasi 53.

Alisema kuwa Paskali alikamatwa mara moja baada ya kushuka katika meli ya m v Matala iliyokuwa ikitokea Bukoba na kuja sengerema huku akiwa amehifadhi bunduki hiyo ndani ya gunua la chumvi na risasi zake akiwa amezidumkiza katika chupa ya maji ya dasani.

Kamanda Barlaw aliendelea kutowa ufafanuzi wa matukio mengine ya kukamata bunduki na kusema kuwa mnano februa 4 mwaka huu katika mitaa ya Igoma jiji hapa jumla ya SMG mbili ambazo hazikuwa na namba pamoja na risasi 11 zilikamatwa.

Alisema kuwa katika tukio hilo majambazi 12 walikamatwa na wengine wameisha fikishwa mahakamani kujibu mashitaka yao.MWANANCHI

No comments: