Thursday, February 9, 2012

YANAYOSEMWA JUU YA MTENDAJI MKUU WA WIZARA YA AFYA

Angalizo:

Haya ni maoni na mitazamo ya watu juu ya utendaji wa baadhi wa wakubwa/viongozi wizara ya Afya kufuatia mgomo wa madaktari unaoendelea. Blogu hii haina uthibitisho kamili juu ya taarifa hii na ushahidi kamili dhidi ya mlengwa (Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya) na haihusiki kwa namna yoyote ile na taarifa iliyotolewa kupitia kiunga cha habari ama chanzo cha habari.


Na Tumbiri,


Kama nilivyohaidi, nimeendelea kuwasiliana na watumishi wa Wizara ya Afya na wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu Ufisadi wa Blandina Nyoni. Yafuatayo ni baadhi ya vitendo vya Ufisadi vya Mama huyu ambaye kwa wengine wanamuona
kama mchapa kazi hodari asiyekuwa na doa na anaezuia mianya ya wizi:-


1. Amekuwa akilipwa mshahara wa ziada na Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) wakati tayari serikali inamlipa mshahara wa ngazi ya Commissioner kupita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)2. Ametengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na afisa manunuzi wake badala yake ame centralize kwake mwenyewe. Kwa maana hiyo, manunuzi yote ya Wizara anamlazimisha (Comand) Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi kumpa kazi zote ndugu yake anaeitwa Donatha Koko.3. Amekuwa akicomand wizara kununua uniform za madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na Maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za manunuzi.


4. Katika mikutano yote inayofanyika Wizarani, amekuwa akicomand kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa tenda ya kulisha chakula washiriki tangu alipotua Wizarani kama Katibu Mkuu.


5. Miezi mitatu iliyopita aliiteua kampuni ya Soft tech ambayo yeye ni mbia kwenda kukagua Accounts System ya Muhimbili kinyume na kanuni za kikaguzi kwa kuwa tayari ana ‘Conflict of Interest’


6. Amekuwa akiongoza Wizara kwa kutumia Informers ambao kazi yao kubwa ni kumpelekea habari nani anasema nini na nani anasema nini kuhusu yeye binafsi na uongozi wake. Informers wake wakuu ni Elias Mkumbo ambaye ni dereva na Donatha Koko ambeye ni ndugu yake wa damu damu na ni afisa ugavi wa wizara


7. Amemkopesha gari la serikali aina ya Suzuki Informer wake Elias Mkumbo (dereva) ambae kimsingi hastahili kukopeshwa gari kutokana na cheo chake. Kwa dereva wa serikali, anachoruhusiwa kukopa ni Baiskeli, Piki piki na Piki piki ya miguu mitatu (Bajaj)


8. Amenunua vingamuzi vya magari manne kwa shilingi 1.3 Billion bila kufuata taratibu za manunuzi kwa kucomand Single source procurement kutoka kampuni moja yenye makao yake huko Israel. Manunuzi haya yamefanyika wakati Hospitali nchini zikiwa hazina dawa, Interns doctors hawajalipwa mishahara yao, watumishi wake wakidai fedha za likizo, uhamisho na vyuo vingi vya afya vilivyo chini yake vikiwa na madeni lukuki.


9. Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010 alihamisha kiasi cha Shilingi 1,968,475,931 mali ya Wizara ya Afya kwenda National Institute for Medical Research (NIMR) bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizi zilikuja kuhojiwa na CAG katika ripoti yake ya serikali kuu ya mwaka 2009/2010


10. Mwishoni mwa mwaka huo huo wa fedha alihamisha kiasi cha Shilingi 3,083,400,000 mali ya Wizara ya Afya kwenda Health Sector Development Project bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizo pia zilihojiwa na CAG.


11. Amelikosesha Taifa kupata fedha za Mfuko wa dunia mzunguko wa 11 (Global Fund Round 11) kwa kupitia Mradi wa Taifa wa kudhibiti Malaria Nchini (NMCP) kwa kushindwa kutumia fedha zote zilizotolewa na mfuko huo katika mizinguko ya nyuma. Kwa kifupi ni kwamba Global Fund hawatoi pesa wakiona una Significant unspent balances.


12. Amekuwa akizuia uhamisho wa Chief Accountant (Bi Helen Saria Mwakipunda), Chief Internal Auditor (Bi Anna J Mhere) na Director of Adminstration and Personnel (Bi Tabu Chando) kwa kile anachodai wanamsaidia katika utendaji wa Wizara. Amezua barua za uhamisho za Chief Accountant mara mbili, Chief Internal Auditor mara moja na Director of Administration and Personnnel mara moja. Ukweli ni kwamba amekuwa akizua uhamisho wa wakurugenzi hawa kwa sababu ni watu waoga na wamekuwa wakikubali chochote anachosema hata kama kinavunja kanunu na taratibu za serikali mfano katika maeneo ya Manunuzi.13. Amemuhamisha aliyekuwa Kaimu wa Kitecho cha Ugavi Mzee Funga kwenda Hospitali ya Mirembe kwa kukataa kununua Uniforms, suti na Maua kutoka kwa Mariedo kwa sababu alihoji ni kwa nini Mariedo watoe huduma wakiwa hawana Mkataba na hawajashindanishwa.


14. Amekuwa akihama hama na dereva wake toka Hazina alipokuwa Muhasibu Mkuu wa serikali hadi Wizara ya Maliasili na Utalii kama Katibu Mkuu. Pia amehama na dereva huyo huyo kutoka Maliasili hadi Wizara ya Afya kinyume na taratibu na kanuni za Utumishi wa umma ambazo haziruhusu kiongozi au mtendaji yeyote wa serikali kuhama na dereva au / na secretary


15. Hamsalimii Naibu wake Waziri Bi Lucy Nkya kutokana na Naibu huyo kugoma kupangiwa dereva ambaye ni Informer wake. Hadi leo hii hamsalimii hata wakikutana kwenye kordo. Kinachowazungumzisha ni madokezo tu.


16. Akiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, aligombana na Waziri wake Bi Shamsa Mwangunga na wakawa hawasalimiani hata wakikutana kwenye kordo

17. Alipokuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali alikuwa anateua ndugu zake na watu anaofahamiana nao na kuwapa vyeo vya u Chief Accountants na Chief Internal auditors bila kuwa na sifa kamili za kuhold CPA (T) na Masters.

18. Yeye ndiye chanzo cha masahibu yanayowakabili Watanzania hivi leo kwa kukosa huduma ya afya kwa kitendo chake cha kutaka kulipiza kisasi kwa Intern Doctors kwa kuwahamishia Mikoani pale walipodai haki zao ambazo ni stahili zao halali

Note: Orodha itaendelea kuongezwa kadri tunavyozidi kupata data kwa watu walio karibu na Wizara


UPDATES ZA KIKAO CHA WAZIRI MKUU NA MADAKTARI , MADAKTARI BINGWA NA MADAKTARI WASTAAFU KILICHOFANYIKA LEO MUHIMBILI

  • Interns warudi muhimbili
  • Madaktari wapewe nyumba na green cards lakini hajasema kivipi
  • Call allowance kwa specialists iwe 25000
  • Call allowance kwa madaktari wa kawaida 20000
  • Katibu mkuu na chief medical officer OUT!
  • Mponda na Nkya watashughulikiwa na Rais!
  • Dr. ulimboka kamuomba PM aruhusu madaktari wakutane watoe tamko.JAMII FORUMS

No comments: