Tuesday, February 28, 2012

WALIOSABABISHA MGOMO WA MADAKTARI KUBURUTWA KORTINIGeofrey Nyangóro


WANAHARAKATI nchini wamejipanga tayari kwa kufungua kesi dhidi ya watu wote waliosababisha mgomo wa madakatari uliosababisha watu baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha na wengine kuathirika.
Habari hizo zinakuja wakati zikiwa zimebakia siku tano kwa madakatari kukutana na kufanya tathimini kuhusu utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa kati yao na Serikali katika hatua za kumaliza mgomo huo wa hivi karibuni.

Akiuzngumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Hellen Kijo –Simba, alisema hatua hiyo itakuja baada ya kukalimika kwa mchakato wa uchambuzi wa madhara yaliyotokana na mgomo huo uliodumu wa zaidi ya wiki mbili.
“Sisi wanaharakati wa haki za binadamu kwa kuzingatia matukio, maamuzi na matokeo yaliyojiri kwa kipindi cha wiki mbili tangu kusitishwa kwa mgomo wa madaktari nchini, tumebaini kuwa madaktari wamerudi kutoa huduma kama kawaida.”alisema Bisimba.

Alisema hata hivyo wamegundua kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Hadji Mponda na Naibu wake, Dk Lucy Nkya hawajawajibika na kujutia vifo na madhara waliyoyasababisha kwa wananchi kutokana na uzembe na kushindwa kwao kutekeleza wajibu.

“Tunamtaka Rais Kikwete awafukuze kazi mara moja”alisema Bisimba ambaye pia aliishutumu Serikali kuwa imeshindwa kutekeleza mambo manne yaliyotolewa na wanaharakati katika tamko lao.

Alisema pamoja na mambo mengine, wanaharakati walimtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kutoa taarifa kwa umma kuhusu athari zilizotokana na mgomo huo.“Tuliitaka Serikali itoe taarifa kwa umma kuhusu athari zilizotokana na mgomo, lakini hadi sasa haijatekeleza,” alisema.

Alitaja jambo lingine kuwa ni pamoja na kkuwataka Spika wa Bunge Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai, waombe radhi kufuatia kitendo chao cha kuzima hoja zilizowasilisha bungeni za kutaka mgomo wa madaktari ujadiliwe.

“Tunataka mamlaka zote nchini zitambue ziheshimu na kuwajibika kwa wananchi. Lakini pia tunataka umma wa Watanzania kuamuka na kuunga mkono harakati za kuikumbusha Serikali kuwajibika,” alisisitiza mkurugenzi huyo.MWANANCHI

No comments: