Monday, February 27, 2012

MAMBO 6 YANAYOFANYA ADUI UJINGA KUWATAWALA /KUTUTAWALA WATANZANIA.

  1. Kazi za magazeti ya udaku na mengine yasiyokuwa makini. Haya ni chanzo kikubwa kwa asilimia 80% ya watanzania wanayoyatumia hivyo kuishia kupanda mbegu ya ujinga na hivyo kupelekea kila wiki kuvuna wajinga wengi sana ,pia haya magazeti mengine ambayo yana andika wazo/hisia za mwandishi kuwa ndio tukio na hali halisi (facts) nakuwandio ndoo kichwa cha habari siku hiyo na kuishia kuvuna watu wanajiendesha kutokana na wazo la mtu (mwandishi) badala lake mwenyewe.athari yake ya kazi ya haya magazeti ni kuwa na watu wasikuwa wakuweza kuchangia mada au ajenda kwa kuwa wana taarifaa za watu sio walizojaza kichwani na sio mada/ajenda hivyo ukiwaleta katika mada ni weupe.
  2. Exposure (kutoka nje ya nchi), nchi yetu ni ya uchumi huru lakini watu kiukweli bado tupo tuna fanya na kuishi maisha ya uchumi usio huru (closed economy) watanzania karibia wote waliotoka nje ndio ambao wanaojua mambo na ndoo inasemekana ndoo wenye ushindani katika soko la dunia lakiniasilimi yao ni ndogo sana ,kama ndoo hivi tunahitaji tujiulize je kama tunataka kuendelea wakati wanafunzi wanaofanya exchangeprogramnje ya nchi ni wachache,wanaoenda kusoma ni wachache,kufanya kazi bado ni wachache je tutawezaje kuendele kutoka hapa tulipo?muda sasa umefika kuanza kupeleka ndugu zetu nje ya nchi kwa wingi wakaitangaze na kuleta teknolojia mpya na mawazo tofauti nakusababisha kuwa na taifa la wajanja, inasemekana nchini Nigeria karibia kila Mnaigeria ni mjanja hakuna wa kumdanganya.
  3. Kutokuwa na muda wakufikiri angalau nusu saa kwa siku. Tanzania maeneo ya wazi kwa umma ya kumpuzika ni madogo na machache sana mjini jua kali wiki nzima watu wapo resi na maisha yao litakalotokea kesho au baadaye na liwe, watu wengi ni waathirika wa brain drain, muda wa kufikiri hakuna na kama kam hujafikiril eo kesho kuna mtu atakufikiria na kukutawala. Sasa nini tufanye kwa hili tutenge maeneo mengi ya wazi kwa mapauziko kwa watanzania,elimu kupitia media juu ya umuhimu wa kufikiri tukumbuke kama hatufirii leo kesho mtu atafikiria na kukutawala.
  4. Kusoma vitabu. Kuna msemo wa siku nyingi unasema kama unataka kumficha mwafrika basi weka ujumbe kwenye kitabu, mara zote kama uantaka ukombozi wa kimaarifa basi huna budi kujifunza kutoka kwa wengine na wewe pia ujue nini ufanye ili ulete mabadiliko tofauti, kuna aina tofauti za vitabu kwa watu wa dini vitabu vyao vitakatifu bado hata theluthi hawafikia walio wengi, muda sasa umefika acha kupenda kusikiliza anzan sasa kusoma mwenye ili uwe huru, nunua vitabu kuna vya kukusaidia wewe ufanikiwe kifedha, furaha, siasa, historia za mashujaa mbalimbali, mara ya kwanza utaona kawaida lakini kadri unavyozidi kuendelea kusoma vitabu ndoo yanakuwa maisha yako ya kila siku na kuwa sawa na kuamka mara ya pili.
  5. Mfumo wa elimu na sera. Mfumo wetu unahitaji mabadiliko sana katika hii dunia ya utandawazi,ndio kuna dunia ziliendelea kwa lugha zao lakini mimi sina maana tukitupe Kiswahili bali ni kama tuna cheza mchezo wa makusudi wa kutengeneza matabaka katika jamii, mfumo unahitaji kubadilika mfano masomo yote yanatakiwa kufundishwa kwa kiingiingereza kuanzia chekechea, primary na kuendelea, huwezi kumfundisha mtu kiingereza na wote wakajua kiingereza wakati umri wa wao (kipindi mtoto ubongo wake una elewa zaidi sana umepita yaani kakomaa tayari) ni sawa na mafunzo ya sarakasi kama hukufanya ukiwa mdogo viungo bado havijakomaa ukija ukubwani kama ukifanikiwa itakuwa kwa shida sana na dunia kuanzia China, Japan, Urusi, kote huku sasa watu wanaongea kiingereza, tuanze sasa kujifunza English maaana mambo mengi yameandikwa kwa kiingereza.Wazazi tafuteni shule za English medium wakasome maana taifa la kesho kama hamjafanya hivyo watoto wenu watatupwa nje ya mfumo msifurahie shule za kata ni mtego wa kutengeneza tabaka la tatu kubwa.
  6. Meditation. Meditation ni muhimu sana kwa taifa kama hili, kwa maendele yaliyo bora na kuwa huru meditation inahitajika,mara nyingi tunapata stress tutokapo makazini, mihangaikoni, tuna hitaji meditation ili kuondokana na haya yote, pia kuirefresh akili zetu zianze upya. Kuwa na fikra sahihi.

Kazi inayofanywa na television na redio station, maisha ya siku hizi taarifa ndio ufunguo wa maisha na sio tena elimu ya darasani (formal education) japo kuwa inaumuhimu pia, television na redio station zinafanya kazi ya kusambaza hizi taarifa kwa asilimia kubwa ya watanzania, lakini sio taarifa za kufanya wao wawe bora na wajanja sana katika hiii dunia, kuna siku nilibahatika kutizama kituo kimoja cha television mtangazaji aliyekuwepo pale yaani wewe ndoo unatakiwa umuambie au ndoo umpe data ilikuwa inatia huzuni kwa mtu kupewa mamlaka ya kutangaza halafu hakuna kitu kichwani alichofanya juhudi aweke ili awaaambie watu, tunahitaji kufanya mabadiliko katika vyombo vetu vya habari kuzifanya taarifa za kuwaza kijanja na kisasa na kujenga mtu.

Imeandaliwa na :

Deogratius Kilawe:
Achivers Club-President
Chairman Afri Youth Organization
0717 109 362
Mfanyabiashara Dar es Salaam


No comments: