Friday, February 10, 2012

KERO ZA WANANCHI WA NANYUMBU- MTWARAHaya ni maoni ya wananchi kwa mhariri wa Gazeti la Raia Mwema yanayohusiana na matatizo ya watumishi katika moja ya Wilaya za Mtwara (Nanyumbu). Na nimeyanukuu kama ifuatavyo:-


WATUMISHI WA NANYUMBU TUNANYONYWA POSHO ZETUNdugu Mhariri, MIMI na wenzangu ni watumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu, mkoani Mtwara. Kuanzia Novemba 12, hadi Novemba 15, mwaka huu 2011, tulihusishwa katika kampeni ya chanjo ya surua, matone ya vitamini A na dawa za minyoo.

Huduma kupitia kampeni hiyo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu ilikuwa ikifanyika katika zahanati na vituo vya afya ambavyo ni takriban 17.

Kampeni hii hugharimiwa na Wizara ya Afya ambayo tumepata taarifa za uhakika kuwa, fedha za kampeni husika zilikwishafikishwa hapa Nanyumbu na kwamba, kazi hii ilipaswa kufanywa na watu watano lakini waliohusika hapa wilayani ni watatu tu.

Kampeni hii imefanyika lakini kwa mizengwe inayohusisha malipo ya posho zetu. Kwanza, malipo yetu hayakufanyika kwa siku zote tulizofanya kazi hadi leo hii naandika barua hii kwako mhariri.

Lakini si tu kutolipwa siku zote za kazi, bali pia kiwango cha malipo ni tofauti. Kuna uchakachuaji na hasa ukilinganisha na wenzetu wa wilaya nyingine ambao si tu wamelipwa kwa wakati na kwa siku zote, lakini pia wamelipwa posho wanayostahili.

Kwa wenzetu wa Wilaya ya Masasi, kwa mfano wale waliotoa huduma hii ndani ya vituo vyao vya kazi walilipwa Sh 60,000 kwa siku, wakati waliohusika na kampeni hiii nje ya vituo vya kazi walilipwa Sh 120,000. Kwetu sisi, tumelipwa Sh. 15,000 tu kwa siku na hata hivyo, hatujalipwa fedha zote.

Tunapowauliza kwa nini hatulipwi fedha zilizobaki wanatueleza tu eti kuna mambo hayajakaa sawa. Tuna uhakika fedha zote zimefikishwa halmashauri isipokuwa kuna ulaji umefanyika, ulaji ambao sasa unaanza kuwa mazoea.

Kwa muda mrefu watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu tumekuwa tukisumbuliwa katika suala la malipo ya posho kwa kazi zinazojitokeza kama hizi za kampeni ya chanjo.

Kupitia kwako, tunaomba kuwasilisha malalamiko yetu ili wakubwa katika Wizara ya Afya na wengine Serikali Kuu wamulike uozo huu ndani ya halmashauri hii.

Watumishi Halmashauri ya Nanyumbu
Mtwara


Mwingine akaongezea haya


MAMBO MABAYA YAKO MENGI SII HAYA TU KUNA MAMBO YAFUATAYO KATIKA IDARA YA ELIMU,KUNA 1. SHULE YA SEKONDARI NANGOMBA WILAYA YA NANYUMBU ILIANZWA KUJENGWA MWAKA 2007 LAKINI MPAKA SASA HAIJAISHA NA MKANDARASI AMESHAKULA CHAKE NA KUKIMBIA, WATOTO WANASOMA KATIKA MAJENGO YA TANROAD AMBAYO IKIFIKA MCHANA NI JOTO KALI PAA LIOKO CHINI SANA TUNAOMBA KUFICHUA ILI KWANI SHULE INAJULIKANA IMEKWISHA. 2. KATIKA KIJIJI HICHO HICHO CHA NANGOMBA NANYUMBU, KUNA MRADI MWINGINE WA BWAWA LA TASAF LILIANZA 1990 LAKINI MPAKA SASA HAKUNA KILICHOFANYIKA NA FEDHA HAWAMU MBILI ZIMELIWA, 50,000,000/= 750,000,000/= 3. PIA KUNA NYUMBA ZA WALIMU SEKONDARY NAZO HAZIJULIKANI ZITAKWISHA LINI? TUNAOMBA MUKAFE UCHUNGUZI ILI WAHUSIKA WAJULIKANE.RAIA MWEMA

No comments: