Friday, January 6, 2012

UTABIRI WA HALI YA HEWATAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI


TAHADHARI YA ONGEZEKO LA MVUA MAENEO YA KUSINI MWA NCHI

Msimu wa mvua unaendelea katika maeneo yanayopata mvua mara moja kwa
mwaka (mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Mbeya, Iringa, Morogoro kusini,
Rukwa, Dodoma, Singida, Kigoma na Tabora.)

Katika kipindi cha siku tano kuanzia Januari 5 hadi Januari 10, 2012, mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la rasi ya Msumbiji unatarajiwa kuendelea kuimarika hivyo kusababisha ongezeko la mawingu katika maeneo ya kusini mwa nchi.

Hali hii inatarajiwa kuimarisha makutano ya upepo wenye unyevunyevu katika maeneo hayo, hivyo kusababisha vipindi vya mvua kubwa katika maeneo ya Nyanda za juu kusini magharibi (mikoa ya Iringa, Mbeya na Rukwa), maeneo ya kusini (mikoa ya Ruvuma, Mtwara na Lindi), baadhi ya maeneo ya Kusini mwa mkoa wa Pwani na Kusini mwa mkoa wa Morogoro (Mahenge).
Aidha mvua za kawaida za masimu zinatarajiwa kuendelea kunyesha katika maeneo ya kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida) na magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma na Tabora).

Maeneo ya Pwani ya kaskazini ( mikoa ya Dar es Salaam, Tanga, Pwani na visiwavya Unguja na Pemba), baadhi ya maeneo ya Nyanda za juu kaskazini masharikiyanatarajiwa kuwa na vipindi vya mvua ambazo ziko nje ya msimu.

Mvua hizi zinatarajiwa kuambatana na upepo mkali katika maeneo ya Bahari yaHindi, hivyo watumiaji wa Bahari wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia mwenendo wa mifumo ya Hali yahewa na athari zake na itaendelea kutoa taarifa.
IMETOLEWA NA

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

No comments: