Friday, December 2, 2011

MR EBBO : MSANII WA BONGO FLAVA AFARIKI DUNIA
Habari za kusikitisha zilizotua hivi punde, Kwa masikitiko makubwa tunasikitika kukutaarifu kuwa msanii maarufu aliyejizolea umaarufu kwa kibao chake cha 'Mi Mmasai Bwana' Abel Motika maarufu kwa jina la kisanii "Mr Ebo" amefariki dunia mapema leo hii.

Inaripotiwa kuwa kifo cha msanii huyo kimeacha simanzi kubwa kwa wananchi wa mkoa wa Arusha na Tanga kwa ujumla ambapo ndio mahali alipokulia na kufanya shughuli zake za kisanii.

Msanii huyo alikuwa akisumbuliwa na homa kwa muda mrefu na kutibiwa katika Hospital mbali mbali hapa nchini na nje ya nchi na baada ya hapo aliamua kupata matibabu ya dawa za kienyeji akiwa nyumbani kwao Arusha.

Msanii atakumbukwa kwa nyimbo kama 'Mi mmasai, Boda boda, Bado, Njaa Inauma' na nyimbo nyingine kibao. Pia ni mmiliki wa Studio ya kurekodia Muziki ya MOTIKA Records iliyopo Tanga. Marehemu ameacha mjane na watoto. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi. Amen


2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Marehemu na astarehe mahali pema popeni. Amina.

sisulu said...

apumzike kwa amani