Thursday, December 22, 2011

HADITHI FUPI.


Na Omary Mwenda (Kutoka Facebook),

(Imehaririwa kuendana na uhalisia)

Katika kijiji flani huko wilayani Pangani, mkoani Tanga palikuwawapo mzee mmoja ambaye alikuwa maarufu kwa jina la Mzee Masumbuko, Wananchi walimwamini sana kwa BUSARA na HEKIMA zake. Hatimaye walimchagua kwa KURA nyingi sana za UPENDO na wakampa UONGOZI WA KIJIJI wakiamini mkombozi wao amekuja.

Mara baada ya Mzee Masumbuko kupata UONGOZI ndipo Maisha ya WANAKIJIJI yakaanza kubadilika, bidhaa zote muhimu zikapanda bei, nishati ya mafuta ya taa iliadimika, Mbaya zaidi wanakijiji wakaanza hata kupokonywa ARDHI WALIZOLISISHWA NA MABABU ZAO, Mzee Masumbuko aliingia mikataba mibovu na wageni wakawa wanajichotea MADINI kijijini hapo na kuacha MASHIMO.

MTOTO WA KWANZA wa mzee huyu ambaye alijulikana kwa jina la CHAKUPEWA alionekana akimiliki vitu vingi vya anasa muda mfupi mara baada ya kumaliza masomo yake huku vijana wenzake wakiwa hawana dira pale kijijini, na aliyetokea kuhoji alitishiwa uhai ama kutoweka ktk mazingira ya kutatanishwa.

Mungu si athumani ilitokea ghafla siku moja usiku Mzee Masumbuko akitokea katika kijiji cha jirani akapigwa na Radi na kufariki papo hapo....! Mpaka leo vijana wa kijiji kile HULIRUSHIA MAWE KABURI LA MZEE MASUMBUKO....! Tafakari....!

No comments: