Wednesday, November 9, 2011

VIONGOZI WA CHADEMA KIZIMBANIViongozi wa CHADEMA jana
walipandishwa kizimbani kwa kile kilichodaiwa ni uchochezi na kufanya mkusanyiko bila kibali. Serikali kwa kutumia vyombo vyake imekuwa ikihaha katika kupunguza kasi ya demokrasia nchini kwa kuwaita wale ambao wanatetea maslahi ya wanyonge kama wachochezi. Na hapa sasa waheshimiwa Tundu Lissu na Wilbroad Slaa wameshtakiwa kwa makosa ambayo hata mtoto mdogo aweza kushangaa nia na madhumuni kupunguza kasi ya mabadiliko.

Kwa mtazamo wangu nadhani ungefanyika mdahalo nchi nzima ili tujue Miaka 25 waliyotutawala hawa jamaa (acha ile ya Baba wa Taifa 24) hawa jamaa wana lipi jipya? Zaidi ya dhuluma, unyanyasaji wa wanyonge,Rushwa, Ulanguzi, Ubadhirifu wa mali ya umma, Kujenga Taifa lisilokuwa na maadili kwa kuwa na mfumo koko/"zombie" unaowaweka wao na watoto wao madarakani, ukosefu wa huduma muhimu za jamii, Elimu duni. Ukianza kueleza Listi itakuwa ndefu mpaka utakata tamaa. Wao wanachodai wamefanikiwa ni kuwa na watu wanaoweza kupiga kelele. Tofautisha kati ya hoja na watu wanaopiga kelele za kusifia madudu yao dhidi ya wale wanaojadili masuala ya msingi. Tunaelekea kubaya sana . Tumeshafanywa malofa tayari kilichobakia sasa ni kutugeuza wote kuwa mashoga ama wasagaji hii yote yatokana na utumwa wa fikra na uongozi kushindwa kufanya maamuzi magumu.PICHA: MICHUZI

No comments: