Friday, November 4, 2011

MAONI YA MDAU
NAPATA FARAJA KUONA HAYANa Yusuf Khalfan Yusuf,

Nilikuwa naperuzi kwenye mtandao, hasa nilikuwa naangalia mahesabu mapya ya kodi za kukombolea gari likiagizwa toka nje kupitia TRA-Website.

Nilivyoenda kwa undani nilikutana na maelezo ya ukusanyaji wa kodi kimkoa. Kuna direct na indirect domestic revenue collection regional wise.Hapa tuangalie Direct Tax Collection (Regional wise)-Domestic Revenue for 2010/2011: July 2010-June 2011.Msimamo ulikuwa kama ufuatao:-

S/NO

MKOA

MAKUSANYO (Tsh Milioni)

1

Ilala

58,809.7

2

Kinondoni

32,858.7

3

Arusha

15,101.3

4

Temeke

12,987.0

5

Mwanza

8,905.0

6

Mtwara

7,608.5

7

Kilimanjaro

6,834.2

8

Morogoro

5,359.60

9

Dodoma

3,787.60

10

Iringa

3,471.40

Yah, msimamo ndo huo kiukusanyaji wa mapato/kodi. Kati ya miji/mikoa hiyo kumi utakubaliana na mimi kuwa mji/mkoa wa Mtwara ni wa mwisho kimaendeleo,miundombinu na kielimu pia. Kwa sasa Tanzania ina mikoa 21 (ukiondoa mipya minne) kwa upande huu wa bara. Mikoa mingi iliyobaki inakusanya kodi kati ya million 2,849.7(Tanga) na million 284.2 (Lindi yaani chini ya billion moja).

Hata hivyo mikoa ambayo haiko top-ten, miundombinu ni mizuri, na kwa kweli uwekezaji unaruhusu. Kwa upande wa Mtwara uwekezaji upo, ila bila kuficha, nature tu ya Mwenyezimungu ndiyo imesababisha hayo. Kwa mfano, bila ya gas ambayo ni asilia, bila ya bandari ambayo nayo ni aslia, hivi Mtwara si pangechoka zaidi? Sasa ninachokusudia hapa ni kwamba Mtwara sasa ni potential place for investment.

Mifuko yetu ya jamii inajenga vitega uchumi vingi tu kama Shopping Malls, Hotels na Apartments kule Arusha, Mwanza, Dar, Mbeya nasikia pia na Dodoma(Ingia kwenye mtandao wa Skyscrapercity.com/Tanzania) uone. Hotels , shopping malls zinatakiwa Mtwara tena sana. Wale wazungu wa Ophir wanaotafuta gas/mafuta wanafanyakazi Mtwara wanalala Dar es Salaam, kisa hamna hotel, na siwalaumu ni kweli kabisa. Hivi kweli mwanya huu wadau wa maendeleo hawajaona au hamna wa kuwatonya potential hizo?

Bahati moja ni ile ya Tanzania Strategic Cities Project, ambayo Mtwara na Kigoma imebahatika. Miji mingine ni Dodoma, Tanga, Mbeya, Mwanza na Arusha. Mradi huo unaofadhiliwa na (MKOPO wa) Benki ya dunia utasaidia barabara , Taa za barabarani, magari ya kuzolea taka na maeneo ya kukusanya taka vikijengwa Mjini Mtwara, hivyo kama usimamizi ukiwa mzuri basi manispaa itapendeza. Hivyo chonde LAPF,PPF,PSPF, NSSF na wengine wakainvest return ya miradi yao itapatikana. Mtwara kuwa mkoa wa sita kwa kukusanya kodi ni ishara tosha pesa ipo, hivyo mifuko yetu ikawekeze mahotel kwenye beach zile zenye mchanga mweupe kabisa tena maji hayana sewarage wastes kama Dar. Beach za Shangani, Mikindani, Ruvula, Msanga-Mkuu, Msimbati na uwanda Tambarare wa Msijute panavutia sana.


Mwisho kuna hili la zile kilometa60 za Nyamwage-Muhoro-Somanga mbona haziishi jamaniiiii? Mambo mengi ya mikoa ya kusini yamelala sana kutokana na kipande kile, mtu akija huko mara moja tu akikumbuka adha ya pale, basi anakata tamaaaa.

Kwa heri kwa leo wadai!

No comments: