Tuesday, November 8, 2011

HII SASA IMEZIDI: KERO YA MAFUTA YA PETROLI MTWARA

Hili suala lilianza kama maskhara lakini athari zake zajidhihirisha dhahiri katika maisha ya kila siku. Sasa hivi Lita moja ya mafuta imeruka mpaka shilingi elfu nane za kitanzania (8,000/=) . Mamlaka zimenyamaa kimya kana kwamba hawalioni. Mamlaka za hapa ni kama vile Mamlaka ya Mapato-TRA na ile ya EWURA. Sasa twaelekea wapi kama hali yenyewe ndio hii ya kukatishana tamaa. Sukari bei juu, Mafuta bei juu , bidhaa bei juu, shilingi yashuka thamani wengine wadiriki kusema nchi imewashinda watu waliopewa dhamana. TUTAFIKA KWELI.

No comments: