Wednesday, October 5, 2011

WATANZANIA WAPUUZENI TGNP NI WANAFIKI

Ni wazi nia na malengo ya Mtandao wa Jinsia Tanzania kwa sasa sio tena kupigania ukombozi wa mwanamke. Kwa sasa ni mawakala wa uchafu wa wazungu na upumbazaji wa wanawake na jamii nzima ya watanzania. Matendo yao, mwenendo wao, imani zao, na mitazamo yao vinadhihirisha wazi kuwa nia zao ni hizo. Nitatoa sababu:-

1. Hawa TGNP, juzi tu wamepata upinzani mkubwa toka kwa jamii kuhusu kuwatumia watoto wa wenzao kama ‘’display’’ ya mashoga kwenye tamasha lao. Na kuwapumbaza watanzania(wakubwa kwa watoto waliokuwa wamejazana kwenye tamasha la jinsia) kuwa ushoga ni halali na ni maumbile ya kuzaliwa. Hivi tujiulize, kama kweli wanaamini kuwa ushoga ni halali kwanini wasingehamasisha kwanza watoto wao wawe mashoga?

Tunawajua watoto wao, ni wasomi wazuri na wana nyazifa nyeti kwenye mashirika, na wengine wako shule nzuri wanasoma ili wawe watu wakubwa katika nchi hii. Kwanini wanataka watoto wa watanzania masikini wawe mashoga ilihali watoto wao hawawi mashoga na wanawasomesha hadi nje ya nchi?

Mbona hatuwaoni mashoga waliosoma na wenyekazi nzuri maofisini? Homoni za ushoga ziko kwa Watanzania masikini tu wenye elimu duni na maisha duni? Kama ni umasikini wangewahimiza mashoga wafanye kazi kwa bidii na warudi shule ili elimu iwakomboe. Hawa ni wanafiki na wazandiki. Watanzania tuwaogope TGNP kama ukoma.

2. Wanatetea ushoga kuwa ni maumbile ya kuzaliwa. Sio kweli. Mbona hatuoni ushoga kwa wanyama?mbona hatuoni punda shoga, mbuzi shoga na ng’ombe shoga? Maana sisi wote binadamu ni wanyama na tuna hisia na shauku sawa na wanyama kwenye kujamiana. Kwanini ushoga uwe kwa binadamu tu? tena kwa watoto wa watanzania masikini na sio kwa watoto wa wanaotetea ushoga?

3. Tunafahamu chanzo cha kutetea ushoga sio dhamira zao, wala akili zao. Ni Pesa chafu walizopewa na wazungu wachafu, ili watumike kuua maadili ya watanzania na wavuruge akili zetu kwa manufaa ya wazungu. Tunafahamu fika kuwa shirika la misaada la HIVOS toka Uhalanzi ndilo lililopita kwenye NGOs kadhaa kuwataka wachukue fedha nyingi kwa ajili ya kutetea ushoga. NGOs zinazoongozwa na Watanzania makini na wenye akili timu WALIZIKATAA FEDHA HIZO CHAFU. Hawa TGNP pasipo kufikiri na uroho wa fedha wakachukua fedha hizi nyingi ambazo sasa zinawadharirisha hata utu wao na hadhi yao kwenye jamii. Ni mafidhuli hawa!

4. Niwakumbushe tu watanzania wenzangu kuwa, shirika la HIVOs ni la Waholanzi. Na waholanzi ndio nchi pekee duniani inayohalalisha uchafu wa kila aina kuhusu uchi wa binadamu na ngono za kila aina. Waholanzi wamefikia hatua ya kujenga. Makumbusho ya uchi wa binadamu na biashara ya ngono na kujamiana hadharani” makumbusho hii inaitwa (Sex Museum), iko Jiji maarufu dunia Amstardam.

Waliofika wanasimulia. Pale uchi wa binadamu hauna thamani tena kwa waholanzi(wafadhili wa TGNP). Ni uchafu na udharirishaji wa ubinadamu. Katika makumbusho hayo(ya uchi na ngono) Wanawake wamepangwa kama nyanya sokoni-ni zaidi ya uchangudoa wa sinza na kinondoni-ambao nao ulitoka huko. Ni laana kuelekea mwisho wa dunia.

Tunakoelekea viwanja vya TGNP vitageuzwa kuwa “Sex museum” ya watanzania na wageni. Na inawezekana kabisa wanawake tukaambiwa ni haki yetu kuolewa na mbwa au punda kama wanavyofanya wazungu sasa huko Ulaya. Sijui kama serikali nayo ipo katika hili. TGNP ni hatari kwa mustakabli wa nchi yetu.

5. TGNP wanatufundisha wanawake kudharau waume zetu na hata kuepuka kuolewa. Wengi wamevunja ndoa zao kutokana na mafundisho potofu ya hawa akina mama.

Wakati TGNP wakifurahia wanawake kuvunja ndoa zao na kufarakanisha familia zetu, wao hawavunji ndoa zao. Tena wameolewa na wanaume waliosoma na maarufu hapa nchini, wenye hadhi kubwa na pesa nyingi. Na wale wasioolewa, ni mahawala wa watu wazito katika nchi yetu. Tunawajua.

Kama kweli wanaume ni wabaya kiasi hicho, kwanini wao wanaolewa-wasisagane wao kwa wao? Kwanini wao wanazaa na wanaume haohao wabaya? kwanini familia zao ziko imara? kwanini wanaendelea kuwa mahawala wa wanaume maarufu? Kwanini wasisagane wao kwa wao? Tena karibu nusu ya viongozi na washabiki wakuu wa TGNP ni wake wa ma-profesa, ma-daktari na wenye pesa. Huu sio unafiki?

6. Hawa TGNP wanatufundisha wanawake kulalamika, kusikitika, kujigamba, kiburi na ubabe usio na maana. Badala watufundishe kuthaminiana, kujenga familia bora, kufanya kazi kwa bidii na kujiendeleza zaidi kwa kusoma na kutafuta taarifa ili tupate maendeleo.

Nilifika kwenye tamasha la wazi pale mabibo kwenye ofisi zao. Kila mwanamke anayepanda jukwaani hakuna anachosema bali kujigamba, kunungu’unika na kuonesha anaweza kupambana mfumodume. Kila mwanamke anayongea anaonesha ana nguvu na akili kuliko Mungu. Akitoka kwenye tamasha anaendelea kuwa masikini, anaendelea kubaki na shida na dhiki zake, wao wana neemeka kwa kulipana mishahara mikubwa na posho kibao.

Hata nchi zilizoushinda mfumodume hazikuwafundisha wanawake kusikitika, kiburi, kujigamba na ngebe na porojo nyingi kama hawa TGNP. Bali ziliwaelimisha wanawake na wanaume; wote wakabadilika wakaheshimiana. Wanawake wenzangu, kuwafuata TGNP tunapotea. Turudi kwenye maadili yetu na tujibidiishe kusoma na kusomesha watoto wetu, na kufanyakazi kwa bidii; ili jamii na nchi yetu isonge mbele. Hawa ni waongo.

7. TGNP wanatukana na kukataa kila aina ya mila na desturi za mwafrika. Maadili na miiko yetu ya asili ambayo ni mizuri tu wao wanaipinga. Kila aina ya mahusiano wanakataa. Mfano, wanapinga mgawanyo wa kazi, wanapinga ndoa za wake wengi, badala yake wanahimiza ushoga na usagaji.

Wanapinga hata dini zetu za asili na za kigeni. Kwao Bibilia na Quran ni vitabu vichafu. Kwa hawa TGNP wao hata Mungu hayupo. Huu ndio mtazamo wa wazungu kwa sasa, japo walizileta dini hizo sasa wazungu wengi hawasali kabisa, sehemu nyingi za Ulaya makanisa yamebaki makumbusho. Mnaokwenda Ulaya mnajua!

8. Watu kama hawa wanaokataa kila iana ya mila na desturi na kuhamasisha uchafu, chuki na visasi, hawafai katika jamii. Ni kweli dini hazina manufaa kabisa kwa jamii? Mbona makanisa na misikiti imejenga mashule mengi-na baadhi ya hawa akina mama wamesoma katika shule hizo? Na baadhi watoto wao hadi leo tunawaona kwenye shule za makanisa? Mbona makanisa na misitiki imejenga hospitali nyingi, vyuo vya ufundi, na kutoa misaada kwa watoto yatima kibao?

Wao TGNP tangu waanze wanaweza kujisifia kwa lipi? Wanapata pesa nyingi chafu kwa wazungu lakini hawajafanya chochote mbali na kuweka matamasha ya kutukana na kuwafundisha watanzania ushetani wa wazungu. Tusiwafuate tutapotea! Mapungufu tunayoyaona kwenye dini zetu yanaweza kurekebishwa. Hawa ni hatari zaidi kuliko sumu.

9. TGNP wanaimba kila siku eti rasilimali za nchi zinawanufaishe wanawake waliopembezoni. Mbona rasilimali zao chafu hawazipeleki kuwanufaisha wanawake wa pembezoni?

Wanajidai wanatetea maji vijijini lakini hawajawahi kuchimba kisima hata kimoja huko vijijini. Eti wanatetea uzazi salama hawajawahi kupeleka hata kidonge kimoja kwa wanawake wajawazito vijijini. Wanatetea ardhi kwa wanawake-hawajawahi hata kufika vijijini kuona kama wanawake hawana ardhi.

Mambo yao yote yanaishi Dar es salaam-kwenye wanawake wachache sana. Hawaendi vijijini. Wao ni Dar es salaam na Ulaya tu kwa wafadhiri wao. Waulize walitumia sh ngapi kuendesha Tamsha lao na kulipana posho na mishahara? Hizo pesa zingechimba visima vingapi ambavyo vingewasaidia wanawake wanaotaabika kutafuta maji? Maneno matupu hayavunji mfupa.

Mwisho, TGNP wamepoteza dira, mwelekeo na kwa sasa hawana malengo. Kama kweli wanayotetea yamo mioyoni mwao, tuwaone sasa wao kwa wao wanasagana; watoto wao wawe mashoga na waletwe display kwenye tamasha. Waende vijijini wakachimbe visima, wajenge zahanati za mfano, na wawanunulie matrekta wanawake wakulima vijijini.

Wakifanya hivyo, tutajua wana maanisha wanachokisema. Vinginevyo, hawa ni wakuepuka kama ukoma. Ni kikundi kichafu, cha kupandikiza uchafu wa wazungu na kuua akili na maadili yetu. Wanafaa kuwa gerezani wanatumikia kifungo cha maisha na sio kuwa eneo la Mabibo lililotakatifu kwa Watanzania halisi. Watanzania Tuwakatea Hawa Vibaraka wa Shetani!!

Imeandikwa na
Asha Maganga,
0714-932374.

WAVUTI


No comments: