Wednesday, October 19, 2011

VURUGU ZAIBUKA BAADA YA KESI YA UCHAGUZI UBUNGE MTWARA MJINI

Vurugu katika viunga vya soko kuu la Mtwara ziliibuka jana mara baada ya uamuzi kutolewa na mahakama juu ya shauri la kupinga uchaguzi wa ubunge Mtwara mjini baina yamgombea wa CCM (mlalamikiwa) na CUF(mlalamikaji). Mara baada ya hukumu hiyo kutolewa, ambayo CCM ilishinda, wafuasi wa CUF walitoka kwa ghadhabu na kuelekea eneo la soko kuu ambako inasemekana kuna duka la mwenyekiti wa CCM mkoa kwa nia ya kwenda kumdhuru lakini hawakufanikiwa. Inaelezwa vitu kadhaa vimepotea pamoja na fedha na mali. Tayari jeshi la Polisi linawashikilia watu kadhaa wanaohisiwa kuhusika na vurugu hizo.

No comments: