Wednesday, October 26, 2011

SHULE YA NDWIKA YAADHIMISHA JUBILEE YA MIAKA 100

Mgeni rasmi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mheshimiwa Anne Semamba Makinda akiwa na wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari ya Ndwika iliyopo wilay a ya Nanyumbu mkoa wa Mtwara. Shule ya Ndwika inatimiza miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1911. Mama Makinda alipatia elimu yake ya Sekondari katika shule ya sekondari ya Ndwika. Mama Makinda ametoa wito wa kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Cha Wanawake.


Mtazamo wangu

Kauli za Wanasiasa ni kama upepo unaovuma. Leo utasikia hiki kesho utasikia kile maisha yanaendelea. Tanzania zipo shule nyingi ambazo viongozi wake wamepita lakini sasa hivi ni magofu. Hakuna anayejali. Waulizwe wao watoto wao wanawasomeshea wapi.

PICHA: MICHUZI

No comments: