Tuesday, August 16, 2011

SERIKALI YATAKIWA KUSITISHA UCHIMBAJI WA URANIUMGeofrey Nyang'oro na Mary Mahundi

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeitaka serikali kusitisha uchimbaji madini ya uranimu katika Wilaya za Bahi, mkoani Dodoma na Manyoni mkoani Singida, ili kuepusha maadhara kwa wananchi.

LHRC pia, imeitaka serikali kusitisha uchimbaji madini hayo katika Wilaya ya Namtumbo mkoani, Ruvuma hadi hapo itakapothibitisha kuwa ina uwezo wa kuzuia madhara yatoweza kutokea.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Slaam jana, Mkurugenzi wa Sera na Maboresho katika kituo hicho, Hanold Sungusia, alisema uchimbaji wa madini hayo ni hatari kwa sababu yana kemikali zenye madhara kwa binadamu na viumbe vingine hai."Madini ya uraniamu ni moja ya kemakali katika kundi la metali ambayo ni hatari kwa usalama wa afya za watu," alisema Sungusia.

Alisema madini hayo yanatoa mionzi na yanaweza kubadilika kwa haraka na kusababisha athari kubwa kwa binadamu na viumbe vingine.Sungusia alitaja athari zinazoweza kusababishwa na madaini hayo kuwa ni ugonjwa wa saratani ya figo, ubongo, magonjwa ya moyo, kupunguza kinga mwilini, vifo vya watoto wadogo na kuharibuika kwa mimba.

Magonjwa mengine ni kupungua kwa nguvu za kiume, watoto kuzaliwa wakiwa na uzito mdogo na kuathiriwa kwa chembechembe za uzazi za urithi."Kwa kuzingatia athari hizi, kituo kinaitaka serikali kuachana na mpango wa kuchimba madini hayo katika Wilaya za Bahi na Manyoni na pia kusitisha kazi hiyo katika Wilaya Namtumbo hadi hapo itakapothibitisha kuwa ina uwezo wa kuzuia madhara hayo,"alisema Sungusia.

Akizungumzia utifiti wa madini hayo, alisema umebaini kuwa kazi ya utafiti inayofanywa na kampuni za Mantra (T)LTD na Uranex (T) LTD, katika maeneo ya Namtumbo, Manyoni na Bahi zina upungufu ukiwamo wa kutoshirikisha wananchi wa maeneo hayo.

"Wananchi hajaelimishwa na kuhadharishwa kuhusu taathira na athari zitokanazo na madini haya ya uranium kwa afya zao, mifugo, mazao,na mazingira kwa jumla,"alisema Sungusia.Katika hatua nyingine, Sungusia ameitaka serikali kusomesha Watanzania katika taalumu hiyo ili iwezi kuwatumia katika shughuli za utaifiti wa madini badala ya kutegemea wageni ili kuwa na watendaji wazalendo.MWANANCHI

No comments: