Monday, August 15, 2011

AJALI YA BASI YATOKEA LINDI

Zaidi ya abiria 18 walikuwa wakisafiri kwa basi la kampuni ya Country Express lenye namba za usajili T 806 AVM wamejeruhiwa vibaya na kunusurika kifo baada ya basi hilo kugongana uso kwa uso na Lori katika eneo la kijiji cha Mnimbila wilaya ya Lindi vijijini mkoani Lindi.

Ajali hiyo imetokea jana jioni na kuwa majeruhi wote wa ajali hiyo hali zao ni mbaya na wameondolewa katika hospitali ya mkoa wa Lindi na kupelekwa Hospital ya Rufaa ya Nyangao kwa matibabu zaidi.


No comments: