Monday, July 25, 2011

PUMZIKA KWA AMANI PROF.

Jumuiya ya Wanataaluma hususan idara ya masuala ya Utawala na Siasa pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, imepata pigo kwa kumpoteza mmoja wa waasisi na waanzilishi wa idara pamoja na kitengo cha sayansi ya jamii na sanaa Profesa Samuel Mushi. Profesa Mushi amewafundisha tuseme wote ambao wamebakia katika idara ile ambao nao ni maprofesa na madaktari katika idara ile na Makamu Mkuu wa chuo kikuu cha Dar es Salaam akiwa mmoja wao. Hili ni pigo pia kwa wanaofuatilia masuala ya siasa ya nchi hii kwa sababu Profesa Mushi alikuwa ni mchambuzi mahiri aliyebobea katika masuala ya sayansi ya siasa. Sina la kusema zaidi ya kusema "PUMZIKA KWA AMANI" Msikilize kauli yake ya mwisho kwa vyombo vya habari akizungumzia hoja ya kujivua gamba kwa mwananchama mwandamizi wa chama tawala siku za karibuni. Bofya hapa

No comments: