Wednesday, July 27, 2011

HOJA YA MDAU
Hi,

Wadau leo nimeona tujadili kwa ufupi maendeleo ya Mkoa wa Mtwara na kwa kuanzia tutagusa miji miwili mkoani humo
yaani Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Halmashauri ya mji wa Masasi!
Tanzania bara ina mikoa 21(Ukiondoa mikoa mipya ambayo iko kwny mikoa ile ile ya zamani) na kwa maana hiyo kuna miji mikuu ya mikoa hiyo kwenye level za miji,manispaa(Majiji mara nyingi huwa makao makuu huwa moja wapo ya manispaa kama Ilala na Nyamagana kwa mifano). Kwa mantiki hiyo Tanzania ina miji mikubwa ifuatayo:
1.Dar es Salaam
2.Mwanza
3. Arusha
4. Tanga
5. Mbeya
6.Dodoma
7.Morogoro
8.Tabora
9.Moshi
10.Iringa
11.Songea
12.Mtwara
13.Sumbawanga
14.Singida
15.Lindi
16.Babati
17.Shinyanga
18.Musoma
19.Bukoba
20.Kibaha-Mail Moja
21.Kigoma-Ujiji.
Miji minne ya mwanzo imepangwa kwa ukubwa wake.Sasa watu wengi wamekuwa wakisema mkoa wa Mtwara uko nyuma wakilinganisha makao makuu yaani mjini Mtwara na miji mingine. Ukiachia miji 4 ya mwanzo na Mbeya na Moshi na kwa kiasi fulani Dodoma kwa sasa, basi ni mji upi unaweza kuwa na jeuri ya kuuzidi mji wa Mtwara?Kila kitu kipo bandari,Airport(ya 4 kwa ukubwa kwa sasa kwani ile ya Songwe-Mbeya haijakamilika). Unajua sijui ni vigezo gani watu wanatumia kukandia mji wa Mtwara, kwa uhakika ukienda Shnyng,Sngea,Sngd,Bk,Bbt, Mrgr, Kbh S/Wanga hamna chochote cha kuuzidi mji wa Mtwara.

Mji wa Masasi nao ni ktk miji mikuu ya wilaya ambayo ni mikubwa. Hapa unapambana na Njombe,Tarime, Korogwe, Mpanda, Geita na Kahama.
Hii ni miji ambayo kimsingi ni wilaya ambazo zimepata hadhi ya kuwa Halmashauri. Sasa huo umaskini watu wanaosema kuwa unatisha Mtwara unatoka wapi, ubaya ni watu kuplicise mambo bila hata ya kufika maeneo husika, bahati mi nimesafiri mikoa yote isipokuwa mkoa wa Manyara hivyo naweza kutoa comparison ya maeneo mengi hapa nchini.
Hivyo tujadili kwa ukweli huu, kama mtu ana maoni tofauti atoe!
Siku njema wadau!

No comments: