Monday, May 23, 2011

WATUHUMIWA WA EPA WALAMBWA MIAKA 5 JELAWatuhumiwa wawili wa kesi ya mabilioni ya EPA Bwana Farjallah Hussein na Rajab Maranda ambao ni mtu na binamu yake wametiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 5 leo mahakamani kisutu. Kesi hiyo iliyovuta umati wa watu ilianza kuonekana kusuasua baada ya kuonekana kutokuwa na ushahidi unaoonekana wa kughushi kwa baadhi ya stakabadhi ili malipo hayo kufanyika. Hata hivyo bado kuna baadhi ya wadau hawajaridhishwa na hukumu iliyotolewa huku wakitilia shaka mwenendo mzima wa kesi pamoja na hasara iliyopatikaba serikalini na kuona kwamba hukumu hiyo haitoshi kutoa fundisho kwa watuhumiwa. Habari zaidi zitawajia kupitia viunga vingine vya habari.

No comments: